Na Magreth Magosso,Kigoma
WAKAZI wa Manispaa ya Kigoma Ujiji,wamelazimika kutembea kwa
miguu kutokana na mgomo wa vyombo vya usafiri kwa kile kinachodaiwa hawana sare mpya kwa
mujibu wa Mamlaka ya usimamizi wa usafiri vyombo vya moto nchi kavu na majini (SUMATRA).
Hali hiyo imekuja baada ya SUMATRA kukamata zaidi ya daladala
20 ambazo zinatoa huduma kwa wakazi wa manispaa hiyo kwa dai la kutokuwa na
sare husika wakati wana risiti ya sare hizo ambazo bado hawajakabidhiwa na
mzabuni wa kushona sare hizo hali iliyowalazimu kugoma kutoa huduma kwa umma
ili kero hiyo ifanyiwe marekebisho.
Kwa upande wa Naibu Katibu wa umoja wa wamiliki wa magari kigoma (KIBOA)Hussein Kaliango alisema,mamlaka
imetoa wiki mbili kwa mwenye daladala awe na sare hizo hali inayokwaza mchakato huo kutokana na muda mfupi na wingi
wa wateja.
Kwa nyakati tofauti madereva wa daladala Kalenga Kasaka na Rashid
Juma walisema wanatozwa kiasi cha shilingi laki mbili na nusu endapo hauna sare
hizo sanjari na kukamata gari,hata kama wakionyesha risiti ambazo tayari
wamelipia sare hizo.
Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kamanda wa hapa Frasser Kashai alisema hana mpango wa kutumia mabomu ya machozi kwa
madereva na makonda ambao wapo katika mgomo huo,huku akiwataka wawakilishi
watatu toka kwa walengwa waende kwa katibu tawala wa mkoa ili kuboresha mgomo
huo.
Meneja wa SUMATRA
kigoma Adamu Mamilo alipoulizwa juu ya hilo alisema awali walikaa kikao na
wadau wa vyombo vya usafiri juu ya sare mpya ziwe kamili mwanzoni mwa mwezi huu
na kuingia ndani ya gari la kamanda wa polisi akidai wanaenda kwa katibu tawala
kumaliza hilo.
Baadhi ya abiria Mawazo Mikidadi na Kamongo Sibonja walisema
hali hiyo inathiri shughuri za uzalishaji mali,kutokana na wananchi kushindwa
kufika maeneo yao ya kazi kwa wakati muafaka,huku wakishauri wadau wakae pamoja
kumaliza adha hiyo.
No comments:
Post a Comment