Pages

KAPIPI TV

Tuesday, March 4, 2014

IDARA YA MISITU KIGOMA YAMGWAYA MMILIKI WA KIWANDA CHA CHUMVI UVINZA KWA KUKATA MISITU

Na Magreth Magosso,Kigoma


IMEELEZWA kuwa,idara ya misitu mkoani Kigoma imeshindwa kuzuia ukataji wa miti hovyo katika misitu ya wilaya ya uvinza kwa kuzingatia taratibu, sheria, kanuni  za idara hiyo.

Hatua hiyo imetokea baada ya watumishi wa idara kuwavamia wakulima eneo la KIDEA kata ya Kazuramimba ambalo limetengwa kwa ajili ya shughuli za kilimo ambalo linamiti inayotakiwa kuondolewa ili kuandaa mashamba kwa ajili ya msimu wa kilimo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya viongozi wa chama cha NRA katibu wa chama Taifa Bw. Fadhili Kiswaga na wafanya biashara wa uvunaji wa miti katika eneo hilo kisheria wamesema kuwa ifikie wakati idara husika inatenda haki kwa  wote juu ya taratibu na sheria za uvunaji bila kujali cheo au umaarufu wa mtu  katika uvunaji wa misitu hiyo.

“Kunakiwanda cha chumvi Uvinza ambapo mmiliki wa kiwanda hicho ambaye amekuwa  akisababisha misitu kutoweka kwa kuvuna bila kufuata utaratibu wa kupanda miti mingine katika pori la Chakulu,Kibaoni na Lugufu wilaya ya Uvinza jambo linalochangia uharibifu wa mazingira".Alisema Bw.Kiswaga

Alisema kuwa serikali inafumbia macho kiwanda hicho katika matumizi mabovu ya ukataji  misitu ambapo zaidi ya tani 50 hukatwa kwa siku pasipo idara ya misitu kufuatilia leseni na mkataba wa kiwanda hicho ulioingia na serikali.
 

“Kiwanda kina zaidi ya miaka 15 wahusika wanaogopa kumchukulia hatua mkubwa huyo kutokana na uwezo wake badala yake wanafanya doria ya kamatakamata mikaa ya wafanyabiashara wadogo ambao  ni wakulima wa kata ya Kazulamimba na kuacha kufuatilia takwimu sahihi za ukataji wa miti unaofanywa na kiwanda hicho" alibainisha Kiswaga.

Naye Nicodem Xavery alisema  idara imekuwa ikifanya operesheni bila kuhusisha Wenyeviti wa mitaa na huwatumia askari Polisi wenye silaha za moto hali inayowatisha wadau wa misitu wakimbie hovyo.

“Kukaa mezani ni suluhu ya kupunguza changamoto ya kufukuzana porini waelimishe na si kutishana wakati  eneo  ni la wakulima na maalum la uvunaji wa miti “ alidai Xaveri.

Meneja Misitu Wilaya ya Kigoma Jackson Temu alipoulizwa juu ya kiwanda hicho alisema wapo katika mchakato wa kupata vithibiti na kumwajibisha  kwa mujibu wa sheria ya misitu na kusisitiza anatumia mkataba wa viongozi  wa wilaya husika.

No comments: