WAKULIMA
wa zao la tumbaku mkoani Tabora watanufaika na ongezeko la bei ya zao
hilo huku pembejeo zake zikishuka bei kwa kiwango kikubwa.
Hayo
yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya muda ya Chama Kikuu cha Ushirika
cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU), Hassan Wakasuvi
alipozungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejea kutoka
nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya mguu.
Wakasuvi
alisema kwa muda mfupi ambao Bodi hiyo imekuwepo madarakani imefanikiwa
kufanya mambo mengi likiwemo kusimamia na kuhakikisha wakulima
wananufaika na zao hilo kwa kuuza kwa bei yenye tija.
Alisema
kuwa katika msimu wa kilimo wa mwaka 2012/2013 mbolea aina ya NPK
iliuzwa kwa dola 53.90 ambapo msimu wa mwaka 2013/2014 iliuzwa kwa dola
51.35 ikiwa na tofauti ya dola 2.55.
Aidha
alisema kuwa mbolea aina ya CAN katika msimu wa 2012/2013 iliuzwa kwa
dola 38.60 ambapo msimu wa2013/2014 iliuzwa kwa 33.30 ikiwa na tofauti
ya dola 5.30.
Aliendelea
kufafanua kuwa mbolea aina ya UREA katika msimu wa kilimo wa 2012/2013
iliuzwa kwa dola 46.60 na msimu wa mwaka 2013/2014 kuuzwa kwa dola 34.85
sawa na tofauti ya dola 11.75.
Pia
alisema Confidor ya pakiti katika msimu wa mwaka 2013/2014 iliuzwa kwa
dola 4.46 ambapo katika msimu wa 2013/2014 iliuzwa kwa dola 2.88 ikiwa
na tofauti ya dola 1.58.
Alisema
dawa aina ya Yavikonyo katika msimu wa 2012/2013 iliuzwa kwa dola 28.94
na 2013/2014 ikiuzwa kwa dola 20.60 sawa na tofauti ya dola 8.34.
Wakasuvi
alisema katika kipindi hicho cha bodi ya muda pia walifanikiwa kuokoa
fedha kiasi cha dola za Marekani 236,088.72 sawa na Sh 4,632,844,632
kutokana na tofauti ya bei ya msimu wa kilimo katika mwaka 2012/2013 na
2013/2014.
CHANZO:HABARILEO
No comments:
Post a Comment