Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSPF Bw. Adam Mayingu akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa mfuko huo katika semina iliyoshirikisha waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wadau wa mfuko huo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo na fursa mbalimbali pamoja na mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo ambapo wakuu wa vitengo mbalimbali wameelezea jinsi mfuko huo unavyofanya kazi zake na ukusanyaji wa michango ya wanachama, Mfuko huo umewaasa waandishi wa habari kujiunga na mpango wa hiari ambao una faida kubwa sana kwa mwanachama atakayejiunga na PSPF, Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jengo la Golden Jubilee Towers jijini Dar es salaam.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mamaa
Thauda wa Nguvu kutoka Chanel 5/ EATV ameshiriki katika semina hiyo
hapa akisikiliza mambo muhimu yaliyokuwa yakielezwa katika semina hiyo
Neema Muro Mkurugenzi wa Uwekezaji katika mfuko huo akitoa mada juu ya uwekezaji katika mfuko wa PSPF.
Mkurugenzi
wa Fedha Masha Mushomba akizungumzia masuala ya fedha na ukusanyaji
pamoja na ulipaji mafao kwa wanachama wa mfuko huo.
Andrew
Nkangaa Mkurugenzi wa Tehama katika mfuko huo akizungumzia jinsi
wanachama wanavyoweza kuchangia mfuko huo kwa kutumia mitandao ya simu
na kurahisisha shughuli zao za kila siku badala ya kufuata ofisi za
PSPF zilipo kwa ajili ya kwasilisha michango yao.
Mkurugenzi
wa mtandao wa www.fullshangweblog.com Bw. John Bukuku kulia akiwa na
Mkurugenzi wa 8020fashion Shamimu Mwasha katika semina hiyo
Andrew Nkangaa Mkurugenzi wa Tehama kulia akiweka mambo sawa kabla ya kuwasilisha mada yake katika semina hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo
Mwandishi wa Habari Abdull Saiboko kutoka TSN akisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo
Adam
Mayingu Mkurugenzi mkuu Mfuko wa PSPF akizungumza na kufanya
ukaribisho katika semina hiyo, katika picha kutoka kulia ni Masha
Mashomba Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Gabriel Silayo mkurugenzi
Uwekezaji na kutoka kushoto ni Andrew Nkangaa Mkurugenzi wa TEHAMA,
Mwanja Sembe Meneja wa PSPF na Neema Muro Mkurugenzi Uendeshaji.



No comments:
Post a Comment