Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
JESHI
la Polisi Mkoa wa Singida limefanikiwa kumkamata George James (30)
mkazi wa kijiji cha Mwamagembe tarafa ya Itigi wilaya ya Manyoni mkoa wa
Singida kwa tuhuma ya kumiliki kinyume cha sheria nyara za serikali
vipande 21 vya meno ya tembo.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema wamefanikiwa
kumkamata George februari 13 mwaka huu saa 2.30 asubuhi huko katika
kizuizi cha mazaoa ya misitu na chakula kilichopo katika kijiji cha
Ukimbu kata ya Mgandu,tarafa ya Itigi,wilaya ya Manyoni.
Amesema
mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia gari aina ya toyota hieze T.797 CQL
kusafirisha nyara hizo kutoka kijiji cha Mwamangembe kwenda Itigi mjini.
“Baada
ya kufanya upekuzi makini,vijana wangu waliweza kuzikuta nyara hizo
zikiwa kwenye mabegi mbalimbali yanayotumika kuhifadhia nguo kana kwamba
alikuwa amebeba nguo tu”,alifafanua.
Kamwela
amesema uchunguzi wa awali wa polisi ukishirikisha idara ya
wanyapori,umeonyesha kuwa vipande hivyo 21 vinakadiriwa kuwa vya tembo
wanne,vina uzito wa kilogramu 49 na thamani ya zaidi ya shilingi 43.1
milioni.
Katika tukio jingine,Kamanda huo amesema kuwa wanawashikilia watu watatu kwa tuhuma ya kumiliki misokoto 192 ya bhangi.
Kamwela
aliwataja watu hao kuwa ni Nuru Saimon (38) mkulima mkazi wa Njia
panda,Williad Kajuna (45) na Said Juma (20) wote wawili wakulima na
wakazi wa Majengo Singida mjini.mkazi.
Amesema
watu hao wamekamatwa februari 11 mwaka huu huko katika maeneo ya njia
panda kata ya Mughunga tarafa ya Ilongero wilaya ya Singida.
“Baada ya taarifa ya raia
mwema kutufikia kuwa katika nyumba ya mtuhumiwa Nuru kuwa kuna
bhang,ndipo askari hao walipofika katika nyumba hiyo na kufanya upekuzi
ndani ya nyumba ambapo waliikuta bhangi hiyo ikiwa ndani ya
begi”,amesema Kamwela.
No comments:
Post a Comment