Jaji Mary Shangali akikagua gwaride la askari Polisi siku ya sheria nchini |
JAJI
wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Mary Shangali amelaani vikali vitendo vya
unyanyasaji vinavyofanywa na jeshi la Polisi kwa wanahabari wa mjini Iringa.
Pamoja
na laana hiyo amewataka askari Polisi wawapo katika mahakama yake wazingatie taratibu
za mahakama.
Aliyasema
hayo mara baada ya kupokea taarifa ya kusikitisha inayowahusisha baadhi ya
askari Polisi bila ridhaa yake kumtoa nje ya mahakama na kumfikisha katika
kituo cha Polisi mmoja wa wanahabari wanaofanya kazi zao mjini Iringa.
Mwanahabari
huyo Frank Leonard, alifanyiwa hayo kwa kile kilichoelezwa na askari hao kwamba
alikuwa akipiga picha wakati mahakama hiyo ikiendelea.
Ilikuwa
wakati jaji huyo akisikiliza kesi ya mauaji ya mwandishi wa Channel Ten, Daudi
Mwangosi inayomkabili aliyekuwa askari wa jeshi hilo, Pasificus Cleophace
Simoni.
Kesi
hiyo ilianza kusikilizwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, Februari 13 kwa
kile kilicholezwa na upande wa mashtaka kwamba uchunguzi wake umakamilika.
“Wameitendea
kosa mahakama hii na wamtendea kosa mwanahabari huyo; kazi waliyofanya siyo yao
, inakiuka taratibu za mahakama,” alisema.
Alisema
kama kweli mwandishi huyo alikuwa akipiga picha na kuhatarisha mwenendo wa
shughuli za mahakama, askari hao walichopaswa kufanya nikuandika memo kwake ili
achukue hatua.
“Hawatakiwi
na hawastahili kuingilia kazi nazotakiwa kufanya mimi au viongozi wengine wa
mahakama wakati mahakama ikiendelea” alisema.
Alisema
mahakama inafanya kazi na wanahabari na itaendelea kufanya nao kazi huku
akiwasihi Polisi kuacha kuwabugudhi.
“Siku nyingine mkija na mkaona kuna dalili ya kufanyiwa kama haya aliyofanyiwa mwenzenu tunaomba mtoe taarifa kwangu au kwa msajili wa mahakama ili tuchukua hatua,” alisema.
No comments:
Post a Comment