Kufuatia wimbi na harakati za kutaka kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2015 linavyoendelea kurindima kumekuwa yakizuka maneno mbalimbali kwa baadhi ya viongozi wenye uchu wa kutaka nafasi hiyo nyeti nchini na hivyo kujikuta wakitamkiana kwa kutumia vyombo vya habari maneno yasiyofaa kwa jamii ya watu waelevu.....Hali hii pia ina dhihirisha kuwa kauli za baadhi ya viongozi zipo tayari hata ikibidi kutoa nafsi ya mtu kwa maana ya kumwaga damu jambo ambalo ni hatari sana.....Chakushangaza zaidi idadi kubwa ya viongozi wanaotupiana maneno ya kejeli na ya hatari wanatoka katika Chama cha Mapinduzi bila kujali nafasi walizonazo....Ukweli ni kwamba Tanzania kwasasa inahitaji kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza ikiwa ni pamoja na uwezo wa fedha pia na wala tusidanganyane kuwa eti mtu asiye na kitu ataongoza na kuwa muadilifu.....Bila kusahau wenye fedha tusiwaite MAFISADI wakati hatujui mbinu wanazotumia kujitafutia huo utajiri,kama wewe ulikuwa mvivu wa kutafuta na pengine fedha zako zinaishia kwenye starehe basi huna haki ya kumsakama mwenzio mwenye kipato huo ni UJINGA.....FURSA inapopatikana ina mambo mawili tu aidha itumike vizuri au laa,sasa kazi kwako wewe uliyetumia vibaya nafasi yako hakuna sababu za kuitana majina yasiyofaa,...Eti mara ooo huyo FISADI aaaa FREEMASON,....Itakusaidia nini,kaa kimya kama huna cha kuzungumza,...Rais wa 2015 Tanzania wananchi waliowengi hawataki kumuona anaongea maneno mengi ambayo hayatekelezeki kwahiyo wanahitaji vitendo zaidi kama wewe unahitaji tumpate Rais kwa kutumia midahalo umechemka Mzee hakuna nafasi hiyo,....Kama unataka hivyo basi Rais atoke vyama vya Upinzani kwakuwa wao wanauwezo mzuri wa kuongea na kuchambua mambo kuliko wa chama tawala.......SAMAHANI NI MAONI TU. |
No comments:
Post a Comment