Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone,(wa kwanza kushoto) akipata maelezo
kutoka mkandarasi wa daraja la Mwankoko manispaa ya Singida,Rogers
Mchau(anayenyoosha mkono) juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja kijiji
cha Mwankoko.
Dk.Kone
alilikagua daraja hilo baada ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa,
kulalamika kwamba fedha zinazotumika katika ujenzi huo ni nyingi
hazifanani na daraja lenyewe. Baada ya kulikagua,alikiri kuwa daraja
hilo lina thamani na fedha zilizotumika na kwamba bado kuna zaidi ya
shilingi 192 milioni zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone,akikagua ujenzi wa daraja la kijiji cha Mwankoko manispaa ya Singida.
Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akitoa maelekezo juu ya kuboresha
ujenzi wa daraja la kijiji cha Mwankoko manispaa ya Singida.
Daraja la kijiji cha Mwankoko linaloendelea kujengwa na mkandarasi Rogers Mchau.
Mkuu
wa mkoa wa Singida (kushoto) akizungumza na Meya Mstahiki wa manispaa
ya Singida,Sheikh Salum Mahami wakati alipokuwa akimaliza kukagua ujenzi
wa daraja la kijiji cha Mwankoko.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,ameipongeza Halmashauri ya Manispaa
ya Singida,kwa juhudi zake za kujenga daraja linalolingana na thamani ya
fedha iliyotumika.
Dk.Kone
ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki wakati akikagua ujenzi wa daraja
hilo, ulioanza rasmi desemba 12 mwaka 2011 na ulitarajiwa kukamilika
novemba 14 mwaka 2012.Daraja hilo linaunganisha kata ya Mwankoko na kata
ya Mtamaa.
Amesema
kuwa fedha ambayo imetumika hadi sasa ya zaidi ya shilingi 216.1
milioni,thamani ya fedha hiyo inafafanana kabisa na kazi ya ujenzi
iliyofanyika.
“Kwa
kweli mmefanya kazi nzuri pamoja na mkandarasi wenu.Fedha ambazo
mmeziomba serikali kuu ili mmalizie ujenzi wa daraja hili,tutakuwa nyuma
yenu katika kuhakikisha mmezipata,ili ujenzi uweze kukamilika kwa
mujibu wa mkataba wenu”,amesema.
Mapema
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Joseph Mchina,amesema mradi huo wa ujenzi
wa daraja hilo,fedha zake zimetoka katika mfuko wa barabara kupitia
OWM-TAMISEMI,zikiwa ni fedha za maombi maalum ya ujenzi wa madaraja.
Katika
hatua nyingine,Mchina amesema hadi sasa ujenzi huo wa
daraja,umekamilika na magari yameanza kulitumia kwa tahadharai,kwani
bado kuna kazi ambazo hazijakamilika.
Mkurugenzi
huyo alitaja baadhi ya kazi ambazo bado hazijakamilika kuwa ni ujenzi
wa barabara ya kuingia na kutoka,mifereji ya wazi kandokando ya barabra
ya kuingia na kutoka na kuweka alama barabarani.
Alitaja
kazi zingine ambazo bado hazijakamilika,kuwa ni pamoja na kazi ya
ujenzi wa kuta za kulinda daraja,kuweka bomba za pembeni na kuweka nguzo
za kuonesha mwlekeo wa daraja.
“Katika
mwaka wa fedha wa 2014/2015,halmashauri ya manispaa,imeomba kiasi cha
shilingi 200 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu”,amesema.
Mkuu
huyo wa mkoa,amelazimika kukagua mradi huo wa ujenzi wa daraja,baada ya
ujenzi huo kulalamikiwa kuwa umetumia fedha nyingi ambazo hazilingani
na kazi iliyofanyika.Mbaya zaidi ni kwamba ujenzi huo upo nyuma ya muda
kwa mujibu wa mkataba.
No comments:
Post a Comment