CHAMA
cha Mapinduzi (CCM), kimejiingiza matatani baada ya kuwapangisha
wafanyabiashara wawili katika flemu moja la kufanyia biashara.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam mfanyabishara Charles Msigwa alisema aliingia
mkataba na Mecy Mziray ambaye kwa sasa ni marehemu na aliendelea
kumlipa kodi ndugu wa marehemu Vesta Haule.
Alisema
wakati akiendelea kufanya biashara katika banda hilo alishangazwa na
viongozi wa CCM tawi la Vigaeni Kata ya Ndugumbi kumfuata wakitaka
aingie mkataba upya na chama hicho.
“Nimekuwa
nikiendesha shughuli zangu za biashara kwa muda wa miaka minne ndipo
nilipofuatwa na viongozi wa CCM na kunishauri nichukue mkataba nao ili
chama kipate mapato,”alisema Msigwa.
Aliongeza kuwa viongozi hao walimuita kwenye ofisi ya tawi na kumuhakikishia hakutakuwa na tatizo lolote juu ya mkataba huo.
“Viongozi
hao waliniambia kuwa mabanda hayo hayarithishwi hata hivyo aliyeachiwa
amekuwa msumbufu wa kodi mwenye banda alishafariki kwa hiyo banda huwa
linarudi na kuwa mali ya chama,”alisema.
Msigwa alisema kuwa aliujaza mkataba huo na kuurudisha ofisini kwao alipotaka kuulipia akawa anazungushwa zungushwa.
“Nilipeleka
malalamiko yangu Kwa uongozi wa Wilaya ambapo uliwaandikia barua ya
kwamaba wanitafutie banda jingine iwapo nikiwa tayari kutimisha masharti
ya kuwa mpangaji wa chama hicho na nilikubali lakini uongozi huo
haukufanya kama ulivyo agizwa,”alisema Msigwa.
Awali
Chama cha mapinduzi (CCM) kiliingia mkataba wa kujenga banda hilo na
Marehemu Mecy Mziray gharama zake na asingeweza kutoka mpaka gharama
zake za ujezi zitakapo malizika.
No comments:
Post a Comment