Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete ambayo kwasasa kuna kila dalili za mgomo baridi unaoendelea chini kwa chini na kusababisha wagonjwa kupata usumbufu mkubwa wakati wanapohitaji huduma za matibabu,Mtandao huu umefanya uchunguzi katika hatua za awali na kubaini kuwa baadhi ya madaktari hawaingii kutoa huduma kwa wagonjwa na hivyo kusababisha wagonjwa wengine kupoteza maisha wakiwa wanasubiria kupatiwa huduma.Hata hivyo baadhi ya Wauguzi na wasaidizi wao wamekiri kwamba ni kweli kuna mgomo uliosababishwa na madai ya maslahi ya wafanyakazi ingawa hawakuwa tayari kutoa ufafanuzi kuhusiana na madai hayo.Baadhi ya wagonjwa wamelalamikia hali hiyo huku ndugu na jamaa waliowaleta wagonjwa wao hospitalini hapo kwa lengo la kupatiwa huduma za matibabu wakiomba Serikali kulishughulikia suala hilo kwakuwa kumekuwa na matukio ya baadhi ya Wagonjwa kupoteza maisha wakiwa kwenye foleni ya kuonana na daktari. |
No comments:
Post a Comment