Pages

KAPIPI TV

Tuesday, November 12, 2013

"MKUTANO WA SHEIKH SHARIFF TABORA YAZIZIMA,MWENYEWE AWAKUBALI WAKAZI WA TABORA,ATOKWA NA MACHOZI YA FURAHA"

Umati  mkubwa uliokuwa ukimsindikiza Sheikh Shariff Mikidadi kutoka viwanja vya Uyui Sekondari eneo ambalo lilikuwa likifanyika Kongamano la dini ya kiislamu kuelekea nyumbani kwao Kiloleni manispaa ya Tabora ulisababisha barabara kadhaa kufungwa kwa muda kutokana na wingi wa watu katika msafara huo ambao wake kwa waume walikuwa wakimshangilia Sheikh Shariff kwa kutaja jina la MwenyeziMungu.Sheikh Shariff alijikuta akitokwa na machozi ya furaha kwa kuona namna watu wanavyomthamini na kumpenda pasipo kujali dini zao.
Licha ya kuwa giza lilianza kuingia umati huu  mkubwa wa watu waukujali suala hilo na hivyo kuliona giza  kama mchana kweupe, wakalazimika kutembea kwa umbali mrefu kutoka katika viwanja vya Uyui Sekondari hadi nyumbani kwao Sheikh Shariff. .
Watu wengi walihitaji kushikana mkono na Sheikh Shariff lakini haikuwa rahisi kutokana na wingi wa watu,wapo waliobahatika kufanya hivyo na kuamini kuwa wamepata neema ya pekee ya mkono wa baraka wa Sheikh Shariff Mikidadi. 
Awali Sheikh Shariff wakati akimalizia na kufunga Kongamano hilo la mwaka 2013 hapa mkoani Tabora alisoma Dua maalumu kuwaombea watu wenye shida na matatizo mbalimbali ambapo idadi  kubwa ya watu walianza kuanguka chini wakiwa wamepandisha mashetani jambo lililoshangaza wengi katika Kongamano hilo lililofanyika kwa muda wa siku tatu.
Sheikh Shariff Mikidadi ambaye ni mzaliwa wa  kata ya Kiloleni  manispaa ya Tabora alikuwa akitumia muda mwingi kuwaasa Waislamu kuwa na umoja na mshikamano lakini kubwa zaidi ni kumcha MwenyeziMungu.
Mmoja kati ya viongozi wa dini ya Kiislam nchini Afrika Kusini Sheikh Salim Dede ambaye anatokea taasisi ya kimataifa ya Islamic Propergation Centre naye alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliofikisha ujumbe katika Kongamano hilo lililoandaliwa na taasisi ya SHEIKH SHARIFF MUSLIM FOUNDATION ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka nchini Tanzania na nje ya Tanzania.
Umati  mkubwa ukiwa umetulia kusikiliza mawaidha ya dini ya kiislamu katika Kongamano hilo.
Sheikh Shariff Mikidadi akiwa jukwaani akitoa mawaidha katika Kongamano hilo lililofanyika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Uyui mjini Tabora.
Baadhi ya wanawake wa kiislamu walikusanyika kwa wingi katika Kongamano











No comments: