Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo la Igalula mkoani Tabora.
Na Mwandishi Wetu
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe
ametembelea kanda ya Magharibi Mkoa wa Tabora na kumfikisha katika jimbo
la Igalula, wilaya ya Uyui.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, Mhe Kabwe amekutana na wananchi katika vijiji vya Goweko, Loya, Miswaki, Miyenze na Kigwa.
Kabwe
amesema wamezungumza kuhusu changamoto ya usafiri wa reli, wafugaji
kunyanyaswa na watendaji wa kata na askari kwa kunyang'anywa mifugo yao,
zao la tumbaku, maji safi na salama na suala la mchakato wa kuandika
katiba mpya.
“Kimsingi
shughuli za kiuchumi za wananchi ni kubwa na hasa Kilimo na mifugo,
hata hivyo ukosefu wa miundombinu unafanya wananchi wasipate thamani ya
mazao yao na jasho la kazi zao,” amesema.
Amesema
alipofika Kijiji cha Loya aliona eneo kubwa lina miti ya mihama ambapo
wananchi wanatumia tu mihama wakati wa njaa na mara nyingi matunda haya
yanaharibika tu yenyewe.
Mbunge
huyo wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amesema lazima matunda haya yawe
na matumizi ya kiviwanda ili kukuza Uchumi na kutoa ajira kwa vijana.
No comments:
Post a Comment