Pages

KAPIPI TV

Monday, September 9, 2013

WATUMISHI WA SERIKALI WALALAMIKIA HUDUMA ZA MFUKO WA BIMA YA AFYA TABORA.

Na Mwandishi wetu Tabora.

Baadhi ya  watumishi wa Serikali waliojiunga na  mfuko  wa  Taifa wa  Bima  ya  Afya  mkoani  Tabora   wamelalamikia kutopata  kwa uhakika huduma  za afya  licha ya kuwa wamekuwa wakichangia  kwa viwango tofauti tofauti.

Akizungumza  na  mtandao huu  mmoja  kati  ya  watumishi  hao  wa  Serikali  ambaye hakutaka  jina  lake  litajwe,alisema  amekuwa  akichangia kiasi  cha  shilingi  52,000 tangu mwaka 2002  lakini  cha kushangaza  amekuwa akisumbuliwa  na  matatizo  ya  macho tangu Julai 2013 na  hivyo  kutakiwa  kupata  miwani yenye  thamani  ya  shilingi  20,000/= lakini hadi sasa amekuwa akisumbuliwa  na kupigwa dana dana.

Hata hivyo  mtumishi  huyo  ambaye  anashindwa  kutekeleza  majukumu  yake  kutokana  na  kukosa  huduma  ya  kupata  miwani  hiyo,amebaisha  kuwa tayari  alikwisha  jaza  fomu  za  maombi  kutoka katika  mfuko  huo  wa  huduma  ya afya  hapa  mjini Tabora  tangu  mwezi  Julai  na  kupata  maelekezo  ya  kupatiwa  huduma  hiyo  katika  hospitali  ya  mkoa  wa  Tabora  Kitete ambako amedai kuwa kumekuwa na  ubabaishaji  usiokuwa  wa  lazima  na  kuleta  usumbufu  mkubwa  kwa  wateja  wa  mfuko  huo  wa  huduma  za  Afya mkoani  Tabora.

Aidha  kwa  upande mwingine  baadhi  ya  wanachama  wa  mfuko  huo  wamekuwa  wakifika  katika  hospitali  na  vituo  vya  afya  wamejikuta  wakipata  usumbufu  mkubwa  wa kutothaminiwa  hatua  ambayo imezidi  kuwasononesha  na kuona kuwa  mfuko  huo  hauna  manufaa  kwao wakati  wanapokuwa na  matatizo  ya  magonjwa.

Mtandao huu unafanya  juhudi  za  kuwasiliana na  uongozi wa  Mfuko  wa  taifa  wa  Bima  ya  Afya  ili  kujiridhisha  kuhusisna  na  kadhia  hiyo  ambayo  kwasasa  ni kero  kubwa  kwa  wanachama  wa  mfuko  huo.     

No comments: