Pages

KAPIPI TV

Monday, September 16, 2013

MTUHUMIWA ADONDOSHA HIRIZI MAHAKAMANI,ALIKUWA AMEPANGA KUMRUSHIA HAKIMU MEZANI

Hirizi iliyokuwa imeandaliwa na ndugu wa mtuhumiwa mmoja wa kesi ya mauaji ambayo alifanikiwa kuishika mkononi kwa lengo la kwenda kumrushia hakimu Mahakama  ya hakimu mkazi Tabora ikiwa ni hatua ya kujinasua katika kesi hiyo ambayo Upelelezi wake umechukua muda mrefu kiasi cha kumfanya mtuhumiwa kutumia hatua nyingine mbadala.Hata hivyo mtuhumiwa huyo ambaye jina tunalihifadhi wakati akiingia  chumba cha  hakimu kwa ajili ya kesi inayomkabili alishindwa kutekeleza adhma yake kama alivyoelekezwa na hivyo kuamua kuitupa chini kabla.Licha ya kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kisheria kuanza kusikiliza shauri hilo lakini mtuhumiwa pamoja na ndugu zake waliamini kuwa chochote kinaweza kufanyika baada ya kuirusha Hirizi hiyo kwenye Meza ya Hakimu.
Mahakama ya hakimu Mkazi mkoani Tabora.


No comments: