Mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza mbio za Kilomita 21 Tabu Mwandu wakati wa Mashindano ya Tabora Marathoni 2013. |
Mshindi wa kwanza Tabora Marathon Tabu Mwandu tayari akiwa anarudi baada ya kufika kituo cha Mwisho Kipalapala akitimiza kilomita 21 na kuibuka mshindi. |
Grace Jackson akikabidhiwa zawadi ya Kikombe baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya Tabora Marathon kwa kukimbia umbali wa kilomita 15 |
Mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya na Waratibu wa Mashindano ya Tabora Marathon wakati ufunguzi wa mashindano hayo. |
SERIKALI
mkoani Tabora imepongeza mashindano ya Tabora Marathon kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa na kwamba itakuwa bega kwa bega katika mashindano yajayo ya mwaka 2014.
Mkuu wa Wilaya
ya Tabora Mjini (DC), Suleiman Kumchaya, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye mbio
hizo akimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Fatma Mwassa, alitoa pongezi hizo kwenye
kilele cha mbio hizo zilizomalizikia kwenye viwanja vya taasisi mjini hapa.
Kumchaya
alisema, amefarijika sana kuona vijana,wazee na watoto wamejitokeza kwa wingi
kushiriki mbio za Tabora Marathon.
Hata hivyo
aliwashauri washiriki wote kuunda vikundi kwenye maeneo yao ili wanapopata muda
wanafanya mazoezi ya riadha na hata mashindano yatakapokuja mwakani wanakuwa
fiti kimwili.
Kumchaya aliwaasa
viongozi wa riadha mkoa wa Tabora, RITAM kwa kushirikiana na Kamati ya Tabora
Marathon, kuanza maandalizi ya mbio za 2014,na baada ya kikao cha tathimini,
wahakikishe wanakutana naye ofisini kwake kuweka mambo sawa kwa mbio zijazo.
Katika hatua
nyingine serikali iliwapongeza wadau walijitokeza katika michango yao,kuwa
serikali itandaa barua za kuwatambua wote kama shukrani kwao.
Wafadhili waliochangia
kufanikisha mbio hizo ni Vodacom Tanzania, Filbert Bayi Foundation, mwanariadha
wa kike, Banuelia Brighton, Meneja mfuko wa taifa wa bima ya afya Kanda ya
Magharibi, Emmanuel Aidan, kampuni ya Tumbaku, ATTT, Mkurugenzi wa GONALLA Phamacy,
Godbless Mafole, Posta, NMB, TRA NHC, MVP, Platnum Credit.
Tabora Marathon
2013, ilishirikisha mbio za Nusu Marathon Kilomita 21 kwa wanaume, Kilomita 15 kwa
wanawake na Kilomita 5 kwa watoto na wazima.
Katika
kilomita 21, mshindi wa kwanza aliibuka Tabu Mwandu aliyetumia saa 1:10.35 aliyezawadiwa
kitita cha sh 100,000, kikombe na medali ya dhahabu, wa pili Dickson Mkami saa
1:13.18 na kujipatia sh 70,000 medali ya fedha huku nafasi ya tatu ikienda kwa
Francis Jombe aliyetumia saa 1:14.36 na kuzawadiwa sh 60,000 na medali ya shaba.
Aidha kilomita
15 wanawake, Grace Jackson alishinda akitumia dakika 55:33.06 na kuzawadiwa sh
100,000, medali ya dhahabu na kikombe, wa pili Maombi Elisha dakika 58:52.01 na
kuzawadiwa sh 70,000 na medali ya fedha huku nafasi ya tatu ikienda kwa Naomi Samweli
aliyetumia saa 1:00.05 aliyejipoza kwa sh 60,000 na medaliya shaba.
Kwa kilomita
5 wanaume wa kwanza aliibuka Robert Mayala wa pili ni Joseph Kimatile na
kufuatiwa na Rashid Malugu waliopata medali za dhahabu, fedha na shaba.
Upande wa
wanawake kilomita tano ni Getruda Musa wa pili Sara Lyimo na Asha Seleman ambao
nao walipata medali, huku mkimbiaji mwenye umri mkubwa Msese Said (65), Msese
Said akipata fedha sh 17,000 kutoka kwa akiwamo DC Kumchaya.
No comments:
Post a Comment