Pages

KAPIPI TV

Friday, April 5, 2013

WANAFUNZI 567 WALIOFAULU DARASA LA SABA SIKONGE WASHINDWA KURIPOTI SEKONDARI

Na Allan Ntana, Sikonge

HALMASHAURI wilaya ya Sikonge, mkoani Tabora, imesema inawasaka kwa
nguvu zote jumla ya watoto 576 ambao walifaulu mitihani yao ya darasa
la saba lakini hadi sasa hawajaripoti shuleni.

Akizungmza na waandishi wa habari, ofisa elimu wa shule za sekondari
wilaya ya Sikonge, Bw.Kiyungi Kasswa alisema kwamba wanafunzi ambao
wamesharipoti shuleni hadi sasa ni 846 sawa na 59%  ya wanafunzi 1,428
waliofanya mitihani ya kuhitimu darasa la saba mwaka jana.

Bw.Kasswa alisema kuwa kati ya watoto 567 ambao hawajaripoti shuleni
wanaume wapo 287 na wasichana 280, huku watoto walioripoti shule
wakiwa wanaume 445 na wasichana 401.

Aidha, Kasswa, alisema kuwa wamejiwekea utaratibu wao ambao utasaidia
kuwapata watoto hao na kuwarejesha shule sanjari na wazazi ama walezi
wao kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Ofisa elimu huyo alisema moja ya mikakati hiyo pia wameagiza viongozi
wote kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji na kata kuhakikisha wanaanza
zoezi la kuwasaka watoto wote na wanaripoti shule haraka kabla ya
mwezi ujao.

Aidha wazazi na walezi hasa jamii ya wafugaji bado hawajaona umuhimu
wa waoto wao kwenda shule na badala yake hutumikishwa kwenye mashamba
ya tumbaku na kuchunga mifugo.

Kasswa anaongeza kuwa kuna changamoto moja ambayo mara nyingi imekuwa
ni chanzo kingine cha watoto kukacha shule ambacho ni umbali mrefu
maeneo mengine watoto wanatembe kilomita zaidi ya 20 hadi 46 toka
ilipo shule na maeneo ya vijiji kwani wanafunzi huhofia usalama wao
hasa kukutana na wanyama wakali lakini wanafanya jitihada za ujenzi wa
hosteli hali ambayo itasaidia kupunguza utoro ikiwemo kupikiwa chakula
hapo shuleni.

Hata hivyo ofisa elimu huyo anasema wamekuwa wakichukua hatua ya
kuhamasisha walimu na wazazi kushirikiana zaidi kwa ukaribu ili
kuhamasisha elimu na umuhimu wake kwa watoto kwa manufaa yao na taifa
kwa ujumla.

Alisisitiza kuwa mipango mingine ni pamoja na wazazi au walezi kutozwa
faini hadi kiasi cha sh 15,000 ili iwe fundisho kwa wazazi wengine
hadi sasa faini hiyo imeanza kuonesha mafanikio na watoto kadhaa
wameanza kurudi shule.

No comments: