Pages

KAPIPI TV

Friday, March 29, 2013

VIGOGO WATATU MANISPAA YA ILALA WANASHIKILIWA NA POLISI KUTOKANA NA GHOROFA KUANGUKA

JKJ5Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Saidi Meck Sadiki katika eneo la  jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam  asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri. JKJ4 JKJ2Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.

Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar-es-salaam linawashikilia watu watatu kutokana na kuanguka kwa Ghorofa hilo.

Kamanda wa Polisi kanda maalumu Suleiman Kova amezungumza na vyombo vya habari amesema licha ya kuwa uchunguzi unaendelea lakini imefahamika watu wawili wamepoteza maisha huku tayari Jeshi hilo linawashikilia watu watatu akiwemo mhandisi wa majengo manispaa ya Ilala,Mkaguzi wa Majengo manispaa ya Ilala na Mhandisi wa manispaa ya Ilala.

Kova amesema watu 17 wameokolewa katika maafa hayo ingawa bado zoezi la uokoaji linaendelea kwa kuondoa kifusi.   

No comments: