Na Allan Ntana,Tabora
MKOA wa Tabora unatarajia kutumia kiasi cha sh bilioni 14.2 kwa ajili
ya matengenezo ya barabara na madaraja katika kipindi cha mwaka wa
fedha wa 2013/2014.
Hayo yamo kwenye taarifa iliyowasilishwa juzi katika kikao cha bodi ya barabara na meneja wa wakala wa barabara mkoa waTabora (TANROAD) Mhandisi Damian Ndabalinze.
Ndabalinze alisema kuwa kati ya kiasi hicho cha sh bilioni 14,249,480,000 kitakachotumika katika ujenzi huo, mfuko wa barabara utatoa kiasi cha sh bilioni 10,179,480 na kiasi cha sh bilioni 4,070,000 zitatoka katika mfuko wa serikali.
Katika taarifa hiyo inaonyesha kiasi hicho cha fedha kitatumika katika
matengenezo ya barabara za mkoa wa Tabora zenye urefu wa kilomita
zipatazo 1,943.34.
Aidha taarifa hiyo inaonyesha kuwa katika kilomita za mtandao huo wa
barabara, jumla ya kilomita 964.80 ni barabara kuu na kilomita 977.54
ni barabara za mkoa.
Aidha meneja huyo wa TANROADS alisema kuwa jumla ya kilomita 158.38 ni barabara za lami na kilomita 1,784.96 ni barabara za changarawe au udongo.
Alisema mkoa wa Tabora unahudumia pia madaraja 286 ambayo yamejengwa
katika mtandao wa barabara hizo.
Akifafanua zaidi Ndabalinze alisema kuwa gharama hizo zitahusisha matengenezo ya kawaida katika barabara za lami, barabara za changarawe na matengenezo maalumu
katika barabara hizo za lami na changarawe.
Aidha alisema fedha pia zitafanya matengenezo ya madaraja,matengenezo
ya madaraja makubwa.

No comments:
Post a Comment