Pages

KAPIPI TV

Tuesday, March 5, 2013

MWANAKWAYA ATAKA KUBAKA MTOTO WA MIAKA SITA -KILOLENI TABORA MJINI

 Askari Polisi Pc Erick akimkabili Gilberth Wiliam ambaye anadaiwa kuwa  mtuhumiwa wa zoezi la ubakaji na kumpeleka kituo kikubwa cha Polisi mkoani Tabora.
 Mtoto wa umri wa miaka sita(jina tunalihifadhi) ambaye ni mkazi wa Kiloleni manispaa ya Tabora ambaye inadaiwa alitaka  kubakwa na Gilberth Wiliam ndani ya Pagala ambapo zoezi hilo lilishindikana baada ya mtoto huyo kukataa na kutoka mbio hadi kwa mama yake mzazi ambako alieleza kwa kina mkasa uliompata.
Humu ndimo Gilberth alidaiwa kutaka kumbaka mtoto huyo.
 
Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Gilberth William(38) mkazi wa kata ya Kiloleni mtaa wa Bombamzinga manispaa ya Tabora kwa tuhuma za kutaka kufanya jaribio la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 6 jina tunalihifadhi.

Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Anthony Rutha amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati uchunguzi wa unaendelea.

Akiongea na mwandishi wetu huko Tabora, Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Bombamzinga Bw. Rajabu Kausimbe alisema alipokea malalamiko kutoka kwa mama wa mtoto huyo na hivyo akalazimika kumuita mtuhumiwa huyo Gilbert na kuanza kumuhoji ambaye awali alikana kuhusika na tukio hilo.

Baada ya mtuhumiwa huyo kukataa  mbele  ya mwenyekiti na baadhi ya wakazi  wa mtaa huo wa Bombamzinga ndipo mwenyekiti akataka kupata ushahidi wa kina kutoka kwa mtoto huyo aliyetaka kubakwa.

Bila kutafuna maneno mtoto  huyo aliweka wazi kuanzia mwanzo namna Bw.Gilbert alivyokuja kumchukua mtoto huyo nyumbani kwao ambako wazazi hawakuwepo kwa wakati huo na kumpeleka kwenye pagala(Jumba bovu) na kumragahai kwa kumpa pipi nne huku akimtaka asiseme kwa mtu yeyote kitendo ambacho angemfanyia.

Hata hivyo ilielezwa kuwa Gilberth hakuweza kutekeleza zoezi alilolikusudia kufuatia mtoto huyo kutokubaliana naye na hivyo kutoka mbio hadi kwa mama yake mzazi  na kuanza kuelezea mkasa uliompata majira hayo ya saa kumi na moja jioni.

Askari Polisi walifika eneo la tukio na kumtia nguvuni mbakaji  huyo huku baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakionesha kulaani kitendo alichotaka kukifanya Jamaa huyo ambaye anafamilia ya mke na watoto katika mtaa huo wa Bombazinga.

Kufuatia sakata hilo baadhi ya wakazi wa eneo hilo wameliambia gazeti hili mtuhumiwa ambaye ni mmoja wa waimba kwaya katika  makanisa ya walokole  kata ya Kiloleni alifanya hivyo kufuatia masharti aliyopewa na Sangoma baada ya kuhitaji apate uongozi kwenye kwaya ya kanisa analolitumikia pamoja na umaarufu katika shughuli hiyo ya uimbaji.


No comments: