Jeshi la Polisi mkoani Tabora limeahidi kuyafungia makampuni
ya ulinzi ambayo yanashindwa kutekeleza
masharti yaliyopewa kwa kuajiri walinzi wasio
waadilifu ambao wamekuwa wakila njama za kufanya uharifu wa wizi kwenye
taasisi ambazo wameingia nazo mkataba wa
ulinzi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP
Anthony Rutha akizungumza
na mwandishi wetu ofisini kwake,alikiri kuwepo kwa baadhi
ya makampuni ya ulinzi ambayo hayafuati taratibu za ajira za walinzi huku akiapa kuyashughulikia
ipasavyo kwakuwa baadhi ya makampuni
hayo yamekuwa yakiajiri walinzi wasio na sifa.
''Ninatarajia kuendesha oparesheni maalumu ya kuyafuatilia makampuni haya ya ulinzi na endapo kama kuna kampuni ambalo halijafuata taratibu na kanuni zilizowekwa tutalifungia haraka"alisema kamanda Rutha
Kuhusu matukio ya hivi karibuni
ya wizi uliofanyika katika Shirika lisilo la
kiserikali la Total Landcare ambalo lilipata hasara ya zaidi ya shilingi mil.kumi baada ya
walinzi wa
kampuni ya ulinzi ya Alliance Day & Night hapa
mjini Tabora ambao
wanadaiwa kula njama na kufanya wizi wa kuvunja ofisi za Shirika hilo,Kamanda Rutha alisema bado Polisi wanaendelea na uchunguzi lakini mlinzi mmoja wa kampuni hiyo anayefahamika kwa jina la Said Kayungilo alitoweka kabla ya kukamatwa.
Rutha alisema wakati wa kufuatilia tukio hilo Polisi ilibaini kuwa pamoja na mambo mengine lakini pia ajira ya mlinzi huyo Said Kayungilo katika kampuni hiyo ya ulinzi ilionesha kutatanisha kwakuwa hata wadhamini wake nao wamekimbia na hivyo kutia shaka kuwa huenda mtandao huo wa wizi umekuwa ukishirikisha walinzi na wadhamini wao katika mashirika wanayoajiriwa.
Alisema kwasasa Jeshi la Polisi litafuatilia ajira ya kila mtumishi au mlinzi aliyeajiriwa kwenye makampuni ya ulinzi ili kujiridhisha kama taratibu zimefuatwa ikiwa ni pamoja na makampuni hayo kuwapeleka walinzi wao ofisi za Jeshi la Polisi Tabora kuchukuliwa alama za vidole ambazo zitapelekwa makao makuu ya Jeshi hilo jijini Dar kwa ajili ya uchunguzi zaidi na ili kubaini kama walinzi wanaoajiriwa na makampuni hayo hawajawahi kujihusisha na makosa mbalimbali ya uharifu.
Hata
hivyo imebainika kuwa baadhi ya makampuni ya ulinzi hapa mkoani Tabora
yameajiri watu ambao hawajawahi kupitia hata mafunzo ya mgambo wakiwemo
walioacha kufanya kazi kwenye baa,mahoteli na kibaya zaidi wengine ni
wale wanaojihusisha na matukio ya wizi wa uvunjaji na tayari taarifa zao
ziko bayana.
Kwaupande mwingine baadhi ya walinzi wanaofanyakazi katika makampuni ya ulinzi hapa mkoani Tabora,kwa masharti ya kutopigwa picha wala kutajwa majina yao walisema tatizo kubwa la wamiliki wa makampuni hayo ya ulinzi ni kupenda kuajiri walinzi kwa mshahara mdogo ndio sababu ya kufikia kuajiri watu wasio na sifa.
Kwaupande mwingine baadhi ya walinzi wanaofanyakazi katika makampuni ya ulinzi hapa mkoani Tabora,kwa masharti ya kutopigwa picha wala kutajwa majina yao walisema tatizo kubwa la wamiliki wa makampuni hayo ya ulinzi ni kupenda kuajiri walinzi kwa mshahara mdogo ndio sababu ya kufikia kuajiri watu wasio na sifa.
"Unavyotuona ndugu mwandishi mishahara tunayoipata ni aibu tupu kutaja mbele za watu,...utakuta kwenye mkataba umeandikwa tunalipwa shilingi elfu themanini,lakini siku ya kuchukua pesa unajikuta umepokea elfu hamsini na tano au arobaini,kisha zinazushwa sababu eti ulichelewa kuingia kazini mara hujapiga pasi sare za kazi,yaani ilimradi tu udhulumike"alisema mmoja wa walinzi wa kampuni la ulinzi la Alliance
''Mdogo wangu najua huwezi kumwambia mtu mimi inafikia hatua usiku naacha lindo nakwenda kuendesha baiskeli ya daladala ili nipate hela ya unga na chai ya watoto asubuhi ninaporudi nyumbani,maana najua kuiba au kushirikiana na waharifu waje wavunje kwenye lindo langu siwezi hivyo nalazimika kutumia njia hiyo ingawa nayo ni kuomba Mungu tu"alisema mlinzi mmoja wa kampuni ya Salu Security ya hapa mjini Tabora.
Pamoja na kuwepo kwa matukio hayo ya uharifu
katika ofisi mbalimbali zinazolindwa na baadhi ya makampuni ya ulinzi,jambo linaloshangaza zaidi ni vipi walinzi hao washiriki uharifu huo na tena kwanini wizi huo uwe ni ule unaohusisha nyaraka na vitu vinavyotunza nyaraka hizo zilizo muhimu.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa baadhi ya makampuni ya ulinzi hapa mkoani Tabora mbali ya kuajiri watu
wasio na sifa lakini pia malipo ya mishahara
kwa watumishi imekuwa ni tatizo sugu
na hivyo kusababisha baadhi
ya walinzi kuwa rahisi kushawishika na kujiingiza katika vitendo hivyo vya kiharifu kwa lengo la kutafuta namna ya kujikimu kimaisha.
Pamoja na kuwa baadhi ya makampuni ya ulinzi kupata dhamana ya kulinda ofisi na mali za taasisi mbalimbali lakini cha ajabu dhamana hiyo imeanza kuingiwa dosari kwa kile kinachodaiwa kuwa ndio yamekuwa mzizi au mhimili mkuu wa vuguvugu la uharifu wa kuaminiwa.
Pamoja na kuwa baadhi ya makampuni ya ulinzi kupata dhamana ya kulinda ofisi na mali za taasisi mbalimbali lakini cha ajabu dhamana hiyo imeanza kuingiwa dosari kwa kile kinachodaiwa kuwa ndio yamekuwa mzizi au mhimili mkuu wa vuguvugu la uharifu wa kuaminiwa.
No comments:
Post a Comment