Anthony Mayunga - Serengeti
MTU mmoja amekufa na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kupigwa
risasi na kuporwa simu na tsh,40,000= mtu anayedhaniwa jambazi katika
kijiji cha Nyamirama kata ya Rung’abure wilayani Serengeti wakitoka
kustarehe.
Tukio hilo limethibitishwa na polisi wilayani hapa na ofisa mtendaji
wa kata hiyo linadaiwa kutokea januari 17,majira ya saa 4:00 usiku
mwaka huu katika kijiji hicho.
Ofisa mtendaji wa kata hiyo Ngeya Alfred alimtaja aliyeuawa kuwa ni
Sore Werema Kihogo(58)mkazi wa kitongoji cha Buhemba kijijini hapo
ambaye alipigwa risasi mbili kifuani na kufa papo hapo.
Majeruhi ametajwa kuwa ni Bwiru Ruhore(33) mkazi wa kijiji cha
Nyarwana kata ya Kibasuka wilayani Tarime ambaye amepigwa risasi
katika paja la mguu wa kulia naamelazwa katika hospitali teule ya
Nyerere ddh kwa matibabu.
Akisimulia tukio hilo lilivyotokea alisema marehemu ambaye alikuwa na
majeruhi ambaye alikuwa mgeni wake wakiwa wanatokea senta ya Nyamirama
kupata kinywaji wakirudi nyumbani ndipo waliposhambuliwa.
“Wakati wanarudi nyumbani kwenye kadaraja walikuta mtu amekaa juu na
kuwaamuru wakae chini…wakahoji kwa nini wakae chini…marehemu alikuwa
na panga katika kuchomoa jambazi akampiga risasi mbili
kifuani”alisema.
Kitendo hicho kilipelekea majeruhi kukimbia na kuruka uzio na kuanguka
,jambazi alimfuata na kumpiga risasi mbili mguu wa kulia na kuanguka
akiwa amepoteza fahamu akampora simu na tsh,40,000= kisha akatokomea.
Alfred alisema majeruhi huyo alifikia kwa marehemu ambaye ni ndugu
yake ,akiwa anamtafuta mke wake anayedaiwa alikuwa ametoroka kwa kwake
.
“Watu walisikia milio ya bunduki na ni katikati ya miji lakini
hawakuweza kutokea kutoa msaada…hata majeruhi alipiga kelele kuomba
msaada hadi asubuhi ndipo watu wakajitokeza”alibainisha.
Naye majeruhi akiongea kwa shida kutokana na maumivu alisema baada ya
kupigwa risasi kwa mwenyeji wake akaanguka chini yeye alipigwa risasi
ya mguu na kuamua kukimbia.
“Jambazi alinifukuza na kunikamata kwa kuwa nilikuwa na maumivu makali
…akanihoji nina nini …nikamwambia nina simu na tsh,40.000=… akasema
nipe…nikampa akaondoka na kuniacha hapo”alisema.
Alisema siku hiyo ndio alikuwa amerudi na mke wake Frola baada ya
kumpatia eneo la Park nyigoti katika shamba la Vedastus Mathayo
akifanya kazi huko,na kuwa januari 18,2013 walitegemea kuondoka ndipo
usiku wakashambuliwa.
Akizungumzia hali ya majeruhi huyo Mganga mkuu wa hospitali hiyo
Dk,Kelvin Mwasha amesema anaendelea vizuri “amepigwa picha imeonekana
mfupa haujapasuka risasi imepiga nyama tu”alisema.
Kuhusu aliyekufa alisema sababu kubwa ni kuvuja damu kwa wingi na
hawakuweza kupata msaada kwa wakati .
Polisi wanadai wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na mke wa
majeruhi alikuwa bado anahojiwa.

No comments:
Post a Comment