Pages

KAPIPI TV

Thursday, January 10, 2013

POLISI DODOMA YAWASHIKILIA 13 KWA TUHUMA ZA KISHIRIKINA


Police1 b1f97
Watu kumi na tatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi  Mkoani Dodoma kwa tuhuma za mauaji yanayohusisha imani za kishirikina.Watu hao wanashikiliwa kutokana na tukio la mauaji lililotokea siku ya Jumatano tarehe 09/01/2013 majira ya saa 04:00 mchana katika kitongoji cha Mtakuja kata ya  Chitemo katika Wilaya ya Mpwapwa.

Katika tukio hilo  walisababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la NELSON S/O NYAGULU mwenye umri wa miaka 32, mkulima wa Chitemo  kwa kupigwa na risasi ya Bunduki aina ya Gobore tumboni na mtu aliyefahamika kwa jina la RASHID S/O KALANI.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba tarehe 08/01/2013 huko katika kijiji cha Chitemo kulikuwa na mnada, ambapo mvua ilinyesha sehemu moja ya kitongoji cha Mtakuja, sehemu ambayo alikuwa  anaishi mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la LEONARD S/O NYAGALU, Miaka 70, Mgogo.
Kwa vile mvua hiyo haikunyesha sehemu kubwa katika kitongoji hicho inasemekana Mwenyekiti wa Kijiji JAVAN S/O MZAZI, Miaka 40, Mgogo, aliibua hoja kuwa kwa nini mvua inyeshe eneo moja tu analokaa Mzee huyo na kuacha kunyesha sehemu nyingine katika eneo hilo na kuwahamasisha wenzake kwenda kwa Mzee Nyagalu akawaeleze vizuri.
Majira ya 23.00 hrs usiku wakakusanyana na kuelekea kwa Mzee  Nyagalu, Walipofika Mzee huyo alisikia watu wakizungumza nyumbani kwake hivyo akavunja ukuta na akatoroka.
Inadaiwa kuwa kundi hilo lililokuwa limeongozana na Mwenyekiti wa Kijiji hicho waliingia ndani ya nyumba na kumkuta mke wa Mzee Leonard Nyagalu na kuanza kumpiga ili aonyeshe aliko mume wake, waliposhindwa kumpata wakabomoa nyumba na kuichoma moto.
Wakati wanafanya tukio hilo, walijitokeza watoto wa Mzee Leonard S/O Nyagalo, mmoja wao akiwa ni NELSON S/O NYAGALU, Miaka 32, Mgogo na ndipo nao wakaanza kupigwa.
Kwa mujibu wa watu walikuwa katika tukio hilo walisema ilisikika sauti ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la RASHID S/O KARANI akisema sasa mmetangaza vita na akafyatua gobore na risasi zikampata NELSON S/O NYAGALU tumboni zilizopelekea kupoteza maisha wakati anapata matibabu.
Baada ya kufyatua risasi toka katika gobole Bw. RASHID S/O KARANI aliwaaga wenzake kuwa anakwenda kujisalimisha Polisi lakini hadi sasa hajaonekana na jitihada za kumtafuta pamoja na silaha aliyotumia zinaendelea.
Majina ya wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na kushiriki katika tukio hilo  ni kama ifuatavyo:-
1.  Dickson S/O Chimosa, Miaka 52, Mgogo, Mkulima na Mkazi wa Chitemo.
2.  Javan S/O Mzazi, Miaka 44, Mgogo, Mwenyekiti wa Chitemo.
3.  Robert S/O Lusije, Miaka 51, Mgogo, Mkulima na mkazi wa Chitemo.
4.  Donald S/O Mponi, Miaka 33, Mgogo, Mkulima na mkazi wa Chitemo.
5.  Daniel S/O Mwamba, Miaka 24, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
6.  Maneno S/O Ngaile, Miaka 36, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
7.  Thomaso S/O Nyagalo, Miaka 28, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
8.  Gilbert S/O Lugaje, Miaka 39, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
9.  Aden S/O Simon, Miaka 33, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
10.      Malolo S/O Sanja, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
11.      Sospeter S/O Sanja, Miaka 35, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
12.      Jocktan S/O Chilomo, Miaka 40, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
13.      Keneth S/O Ngaile, Miaka 38, Mnyamwezi, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.

Aidha siku ya Jumamosi tarehe 05/01/2013 majira ya 08:00 asubuhi kulikuwa na tukio la mauji  lililotokea katika Kitongoji cha Magungu, Kijiji cha Mpendo, Kata ya Mpendo Tarafa ya Kwa Mtoro Wilaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma.
Ambapo mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina la TONY S/O SOKOINE mwenye umri wa miaka miwili na nusu (2.5), mkazi wa Kijiji cha Mpendo alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa kuchomwa na kisu shingoni kilichorushwa na mtoto mwenzake aliyefahamika kwa jina la SOMEI S/O REMENDA mwenye umri wa miaka mine (4) mkazi wa Kijiji cha Mpendo.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha Kifo hicho ni kwamba marehemu na mtuhumiwa walikuwa wanacheza nje nyumbani kwao kwa akina SOKOINE S/O RENENDA ambapo mtuhumiwa alirusha kisu kwa lengo la kumuua ndege aliyekuwa juu ya mti  uliokuwa karibu na nyumba yao, ndipo kisu huchi kiligonga kwenye mti huo na wakati kinadondoka kilimjeruhi marehemu kwa kumchoma shingoni  na kusababisha kifo chake.

DAVID A. MISIME - ACP
                  KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA    

CONTACT:
POLISI MKOA WA DODOMA
DAWATI LA HABARI, ELIMU NA MAHUSIANO,
Phone:  0715 006523, Luppy Kung’alo – Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP)
Phone:  0712  360203, Silyvester Onesmo – Police  Konstebo  (PC)

No comments: