Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya watoto wanaoishi katika kijiji cha Igombe manispaa ya Tabora wakati wa ziara yake hapa mkoani Tabora.
RAIS
wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete amewatoa
hofu watanzania na kusema kwamba hakuna mtanzania yoyote atakaekufa kwa
njaa japo maeneo mengi ya nchi yamekuwa yakilalamikia tatizo la kuwepo
kwa njaa kwa baadhi ya mikoa na wilaya.
Kauli
hiyo aliitoa juzi wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika viwanja vya chipukizi mjini Tabora wakati wa ziara
yake mkoani hapa.
Alisema
kwamba kutokana na tatizo la njaa kwa baadhi ya mikoa serikali ipo
tayari kuhakikisha hakuna mwananchi ama mtanzania atakaye kufa kutokana
na janga hilo.
Alisema
kwamba tayari srikali imejipanga kuhakikisha kila mtu anapata chakula
cha msaada kupitia kamati za mahafa za wilaya kata na mkoa kwa ajili ya
kupatiwa chakula hicho .
Dkt
Kikwete alisisitiza kwamba hifadhi za chakula zilizopo katika mikoa ya
shinyanga kwa ukanda huu inachakula cha kutosha kwa ajili ya wananchi wa
mikao ya ukanda huu.
Hata
hivyo alisema kwamba kama chakula kitakwisha kwenye magahala yan
hifadhi za taifa serikali ipo tayari kuangiza chakula hicho hata nje ya
nchi ili kuakikisha kuna mtu anayejkufa kwa kukosa chakula .
Alisema kwamba licha ya ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa tayari kimefanya tathimini
ya mahitaji ya chakula kwa baadhi ya mikoa na wilaya hapa nchini na
katika maghala ya hifadhi ya chakula na kuonyesha kuwa bado kipo na chakutosha kwa mikoa ambayo imeomba chakula kwa ajili ya wananchi wake .
Rais
kiwete akizungumzia swala la ukimwi alisema bado maambukizi ya ukimwi
yanatishia maisha ya watanzania wengi na kuwataka wanatanzia watumia
kinga kwa ajili ya kufanya tendo hilo.
Alisema
kwamba kitendo cha wananchi wengi nchini kupata maambukizi ya ukimwi na
ukimwi imekuwa si cha dharula bali ni chakujitakia na cha makusudi
kwani kabla ya kwenda kwenye haadi lazima kupanga wapi mkutane na
kufanya kitendo hicho.
Alisema
kwamba sasa kabla ya kufanya inabidi kila mtu hatafute kinga na nani
haje nayo ili kuwaza kujikinga na mambakizi hayo ya ukimwi .
“jamani
hali ya maambukizi ya ukimwi nchini yanatisha lakini basi tumieni kinga
ili maambukizi hayo yasiongezeke kwani kitendo hicho kipangwa muda na
saa sasa nini kinashindikana kununua kinga ili kuwaze kujikinga wote na
maambukizo hayo”.alihoji rais kikwete.
Alisema
kwamba katika kipindi cha januari hadi septemba mwaka jana mkoa wa
tabora jumla ya watu 41,032 walipimwa ,kati hao wanaume 19 ,531 na
wanawake 21,591.
Alisema
kuwa watu 3,136 walikutwa na maambukizi ya ukimwi kati yao ni wanaume
1,324,na wananwake 1820sawa na asilimia 7.6 kwa wale waliopima hali hii
inaonesha bado maambukizi yapo juu.
Dkt
kikwete aliendelea kusema kwamba watu 39,659 wanahudhuria klinik na
kati ya hao watu 20,486 wanatumia dawa na ARVs ambao ni sawa na asilimia
51.6 .
Alisema kwamba kwa hali hiyo ni mbaya sana hivyo kila mmoja wetu anawajibu mkubwa wakujilinda afya yake .
Hata hivyo Rais Jakaya Kikwete amewahakikishia
wananchi wa tarafa ya iloloagulu katika wilaya ya Uyui kuwa swala la
wilaya hiyom kuwa na halmashauri mbalin linawezekana ili kupunguza kero
kwa wananchi hao.
Awali
mwenyekiti wa srikali ya kijiji cha ilolagulu ,Ally Magowa alimwambia
Rais kwamba wananchi wa kijiji hicho wamekuwa wakitembea umabli mrefu kw
ajili ya kupata huduma za kiserikali kutoka hapo hadi Isikizya .
No comments:
Post a Comment