Na Beatrice Masaki-Tabora
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Majija
Kasubi (38) mkazi wa Mirambo kata ya mbugani ameuawa kwa kuchomwa kisu maeneo ya Mwanza
road mjini Tabora.
Akithibitisha kutokea kwa
tukio hilo kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Athony Rutha alisema tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa tarehe 22 januari mwaka huu ambapo Bw. Majija alikuwa akinywa pombe
za kienyeji na ndipo alipochomwa kisu
na mtu mmoja kwenye paji la uso na tumboni jambo ambalo lilisababisha kifo chake baadae wakati akipatiwa matibabu baada ya kufikishwa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete.
No comments:
Post a Comment