“Ni kutoka Bukoba na Biharamulo,wakamatiwa Mugumu,wadaiwa ni mtandao
wa majangili”
Na Anthony Mayunga-Serengeti.
ASKARI polisi wawili na raia mmoja kutoka Biharamulo na Bukoba
wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Serengeti baada ya kukamatwa
na vipande 17 vya meno ya tembo watatu.
Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom
Mwakyoma limetokea januari 6 mwaka huu katika kijiji cha Rwamchanga
na mjini Mugumu .
Watuhumiwa waliokamatwa wametajwa kuwa ni D/c Gerard Tuti mwenye namba
za F5553 ambaye ni mpelelezi katika ofisi ya kamanda wa makosa ya
jinai Bukoba.
Askari mwingine ni D/c koplo David Delina mwenye namba E9172 kutoka
ofisi ya upelelezi Biharamulo na raia Boniphace John Kurwa(31) mkazi
wa Geita.
Askari hao walikamatiwa katika nyumba ya kulala wageni ya Galaxy
iliyoko mjini Mugumu januari 6 majira ya saa 8 usiku baada ya mwenzao
kukamatwa na shehena hiyo na kuwapeleka askari walipo wenzake .
Kamanda alisema askari hao baada ya kuhojiwa walikiri kuwa walifika
hapo kwa maelekezo ya mfanyabiashara mmoja Boniphace Emmanuel(Maarufu
kama Mnyarwanda mkazi wa Biharamulo.
Kukamatwa kwao kunatokana na taarifa zilizotolewa polisi kutokana na
interejensia kali ya shirika la Tanapa kwa ajili ya kukabiliana na
mtandao huo hatari unaundwa na wafanyabiashara wakubwa,na baadhi ya
watendaji wa vyombo vya dola na maamzi.
Ilivyotokea.
Kwa mjibu wa kamanda wa polisi inadaiwa kuwa askari polisi
wakishirikiana na askari wa hifadhi ya taifa ya Serengeti wakiwa
kwenye doria walifanikiwa kumkamata Boniphace Kurwa akiwa na pikipiki
yenye namba za usajili T784 CCC aina ya Sunlog.
Mtuhumiwa huyo akiwa na mwenzake aliyetambuliwa kwa jina moja la
Nyarata ambaye alikuwa na pikipiki yenye namba za usajili T 834 BPH
Toyo ambazo wamiliki wake wanafuatiliwa walikuwa wamebeba nyara za
taifa pembe za tembo vipande 17 kwenye mabegi.
Hata hivyo Nyarata alifanikiwa kukimbia na kutelekeza pikipiki na
mzigo huo na anasakwa ili aunganishwe na wenzake kwenye kosa hilo.
Mwakyoma alisema baada ya kubanwa mtuhumiwa huyo aliwataja askari hao
na kuwapeleka askari hadi nyumba ya kulala wageni ya Galaxy iliyoko
mjini Mugumu na kuwakamata .
“Hao askari walikuja na gari aina ya Toyota Carina yenye namba za
usajili T403BPK inasemekana ni mali ya koplo David”alisema kamanda.
Wasomewa mashitaka kijeshi.
Kwa mjibu wa kamanda huyo alisema askari hao tayari wameishawasomea
mashitaka ili taratibu za kiraia ziweze kuchukua nafasi yake.
“Suala la maamzi ya kijeshi yaliyofikiwa bado…lakini watuhumiwa wote
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani januari 8 mwaka huu,taratibu za
uchunguzi zinaendelea”alisema.
Alidai watumishi wa serikali wanatakiwa kutambua kuwa hawako juu ya
sheria na wale wote wanaotuhumiwa na kuthibitika watakamatwa na
kufikishwa mahakamani kama itakavyokuwa kwa hao.
Habari za uhakika kutoka vyanzo vya habari zinadai kuwa watuhumiwa hao
waliingia mjini Mugumu januari 4 mwaka huu wakiwa na gari aina ya
Toyota Ballon lenye namba za usajiri T403 BJK kutokea Biharamulo.
Uchunguzi wa Mwananchi ulibaini kuwa watuhumiwa hao wakiwa na mwanamke
mmoja walifikia hoteli ya Galaxy ambapo Delina alilala chumba namba
29,na Tuti ambaye alikuwa na mwanamke walilala chumba namba 28.
Hata hivyo Kurwa alikataa kulala hapo baada ya kukosa chumba eneo la
chini lililojitenga na kuwataka wenzake walale ,”huyo ndiye alikuwa
mwenyeji wao alipokosa chumba kule chini alisema hawezi lala hapo na
kuwataka wenzake walale”kilisema chanzo cha uhakika.
“David aliandika kuwa anatokea Bunda kabila lake ni Sandawe na Gerard
aliandika kuwa anatokea Bunda mzaliwa wa Mwanza kabila lake msukuma
,lakini hawala yake hakuandika jina”mwananchi iliambiwa.
Chanzo hicho kilidai kuwa januari 5 ,2013 waliaga kuwa
wanaondoka,lakini kwa muda mfupi walirudi na kuomba vyumba vyao huku
mwanamke waliyekuwa naye akidai mambo yao hayakwenda vizuri ndiyo
maana wamerudi.
“Mwanamke alifua nguo zake huku wale wengine wakiwa wanakunywa pombe
toka asubuhi na kucheza pool….lakini ambaye alikataa kulala hapa
alionekana mwenye pilika pilika…hatukuwatilia shaka hadi saa 7 usiku
polisi wakiwa na huyo Kurwa wakaja akaanza kuwaonyesha wenzake na
kuwachukua”kilisema chanzo hicho.
Askari hao walikuwa kikosi cha kuzuia uharifu Biharamulo.
Habari za uhakika zinadai wakiwa kwenye kikosi cha kuzuia uharifu
wilayani Biharamulo kabla ya Gerald kuhamishwa walikuwa kwenye mtandao
mmoja na mfanya biashara huyo.
Askari mmoja alikuwa likizo.
Habari za uhakika zilibaini kuwa mtuhumiwa mmojaDavid ambaye amepata
cheo cha koplo hivi karibuni inasemekana yuko likizo alitumia muda
huo kufanya kazi za mtandao wake.
Inasemekana kuwa kazi hiyo wanaifanya mara kwa mara kwa madai kuwa
tembo katika mapori ya Biharamulo wameuawa na wamepungua,lakini
hifadhi ya taifa ya Serengeti ni wengi.
Tanapa.
Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi alisema wao wanaomba sheria ichukue
mkondo wake kwa kuwa ujangili unatishia uhai wa wanyama.
“Kazi yetu ni ulinzi wa maliasili hizi hivyo hatutasita kumchukulia
hatua mtu yeyote atakayekamatwa kwa kosa la ujangili,na tunapambana
kuhakikisha huo mtandao wa ujangili unatokomezwa”alisema.

No comments:
Post a Comment