Pages

KAPIPI TV

Tuesday, December 11, 2012

SENENE WASABABISHA WALIMU,WANAFUNZI KUCHELEWA KUINGIA MADARASANI IRINGA


Mvua  kubwa  iliyonyesha usiku  wa  leo katika  mji  wa Iringa  imeshusha neema kwa wakazi wa  mji wa Iringa ambao ni wapenzi  wa  Senene  baada ya  baadhi ya  wamiliki wa nyumba  kudaiwa  kuwazuia wapangaji  wao  kuokota  senene katika nyumba  zao huku walimu pamoja na watumishi  wa umma  wakichelewa  kuingia madarasani kutokana na zoezi la  kukamata senene hao.

Uchunguzi  uliofanywa na mtandao huu katika  shule mbali mbali  za Manispaa ya Iringa asubuhi ya leo umebaini  kuwa idadi kubwa ya  wanafunzi na  walimu  wakia katika mashamba ya  shule  zao na nje ya  vyumba vya madarasa pamoja na  wanafunzi wao wakifukuza senene  wakati katika baadhi ya  ofisi  wa umma kama TRA na maeneo ya majeshi  ya ulinzi  pia  wanajeshi  walinaswa  wakifukuza  senene hao.


Wakati   wazazi wa  wanafunzi hao  wakilalamikia  hatua ya walimu  wa shule za msingi  kuwatumia wanafunzi katika   kuokota senene kwa  upande  wao  baadhi ya  wamiliki  wa  nyumba katika mji wa Iringa wamedaiwa  kuwanyanyasa   wapangaji  wao kwa  kuwazuia  kuokota  senene  zinazoanguka katika  nyumba  zao  kwa madai  kuwa senene  hizo ni mali ya mwenye nyumba na iwapo  wanataka  basi kutoka  nje ya uzio wa nyumba  hizo usiku kwenda kusaka senene mitaani .

No comments: