Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es
Salaam, imetuma timu ya Makachero kuja Zanzibar kuungana na wenzao
wengine wa Polisi Zanzibar katika Upelelezi wa tukio la kushambuliwa kwa
Paroko wa Parokia ya Mpendae Amrose Nkenda.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Zanzibar ACP Yusuf Ilembo, amesema kuwa timu hiyo ambayo inaongozwa na
Afisa mmoja wa ngazi ya juu (hakumtaja jina) ina jumla ya Makachero
watano waliobobea katika masuala ya upelelezi hapa nchini.
Amesema
kuwa nia ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi
Mwema, kuituma timu hiyo kuja hapa Zanzibar, ni kutaka kuengeza nguvu
katika tukio hili ambalo linatazamwa kwa aina tofauti hasa ikizingatiwa
kuwa aliyeshambuliwa ni Kiongozi mkubwa wa dini na limetokea katika
kipindi cha siku kuu ya Krismas.
Amesema
Jeshi la Polisi limeamua tukio hili kupelelezwa kwa pamoja kati ya
wenzao wa makao makuu ya Polisi Dar es salaam na wa hapa Zanzibar ili
kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika katika kumshambulia Paroko huyo
wanakamatwa.
Hata
hivyo kamanda Ilembo amesema kuwabado Polisi wanaendelea na Upelelezi
wa kubaini sababu za kushambuliwa kwa Paroko huyo bila ya kuibwa kwa
kitu chochote kutoka kwa mshambuliwa.
Amesema
kuna uwezekana kuwa watuhumiwa wameshindwa kuchukua kitu chochote baada
ya kubaini kuwa eneo la tukio lisingekuwa salama kwao kwa vile kulikuwa
na walinzi na ni eneo ambalo ni karibu kabisa na makazi ya viongozi
wengine wa dhehebu hilo.
Akizungumzia
siku kuu ya mwisho wa mwaka 2012 na mwanzoni mwa mwaka 2013, Kamanda
Ilembo amewahimiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la
Polisi kwa kutoa taarifa pale wanapobaini kuwepo kwa wahalifu ili
wachukuliwe hatua.
Naye
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma
Mohammed, amewatahadharisha wazazi na walezi kutowaruhusu watoto wadogo
kuranda barabarani ama kwenda katika fukwe za bahari kuogelea pasipo
uangalizi wa watu wazima.
Kamanda
Aziz amesema kuwa uzoefu unaonyesha kuwa watoto wengi wamekuwa
wakigongwa na magari ama kuzama na kufa maji katika siku hizi za siku
kuu za mwisho wa mwaka kwa kukosa uwangalizi wa watu wazima.
Aidha
amewataka wananchi kutoziacha nyumba zao wazi ama bila ya kuwa na
uwangalizi wa kutosha ili kutowapa nafasi kwa wahalifu kupata fursa ya
kuwaiba.
0715 886488, 0867 886488, 0784 886488, 0774 886488 Insp. MHINA
No comments:
Post a Comment