Jengo la Benki ya CRDB Burundi. (Picha zote kwa hisani ya Dar es Salaam Yetu Blog na This Day Magazine).
Rais
wa Burundi Piere Nkurunziza akiwasili katika sherehe za ufunguzi rasmi
wa Benki ya CRDB jijini Bujumbura, Burundi. Benki ya CRDB imekuwa Benki
ya kwanza ya kizalendo kufungua tawi lake nchini Burundi.
Rais
wa Burundi, Mheshimiwa Piere Nkurunziza akikata utepe kuashiria
ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB nchini Burundi Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
Rais
wa Burundi Mheshimiwa Piere Nkurunziza akisalimiana na Mkurugenzi wa
Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB Tully Esther Mwambapa alipokuwa
akiwasili katika sherehe hizo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na Balozi wa
Tanzania Nchini Burundi Dk. James Nzagi (Kushoto) na Katibu wa Benki
hiyo Bwana John Rugambo (wa pili kushoto) na Meneja Mkuu wa Benki ya
CRDB Nchini Burundi Bw. Bruce Mwile.
Rais wa Burundi Mheshimiwa Piere Nkurunziza akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB nchini Burundi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzano kutoka Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment