Na Allan Ntana, SIKONGE
Kukosekana kwa mvua za kutosha mwaka huu kwa baadhi
ya maeneo mkoani Tabora,
Hayo yalibainishwa katika kikao cha baraza la
madiwani la halmashauri ya wilaya ya Sikonge kilichofanyika juzi wilayani hapa katika
ukumbi wa chuo cha maendeleo ya wananchi Sikonge FDC, ambapo madiwani
walitaarifiwa juu ya kukauka kwa bwawa hilo la mradi wa umwagiliaji na hivyo
kufanya shughuli zote za kilimo kusimama.
Akitoa taarifa mbele ya baraza juu ya hali halisi ya
bwawa hilo la mradi wa umwagiliaji, unaotegemewa sana na wakazi wengi wa vijiji
vya Kisanga, Ulyanyama, Ufisi na vijiji jirani katika kilimo cha mpunga, Kaimu
mhandisi wa idara ya maji wilayani hapo Bw. Wibonela Jafari, alisema kuwa bwawa
hilo limekauka kabisa na yamebakia matope sehemu zilizo nyingi.
Aidha Bw. Jafari alisema kuwa kukosekana kwa mvua za
kutosha mwaka huu kumeathiri sana shughuli za kilimo katika maeneo mengi na hasa
kwa wakazi walio katika ukanda wa bonde hili la Ulyanyama, na kuongeza kuwa kwa
sasa hivi hakuna maji kabisa, hivyo hakuna kilimo kinachoendelea.
Bw. Jafari alitaja athari mbalimbali zinazotokana na
hali hiyo kuwa ni kukwama kwa shughuli zote za kilimo cha umwagiliaji, kukwama
kwa mipango ya halmashauri ya kutumia bwawa hilo kusambaza maji kwa ajili ya
matumizi ya nyumbani katika vijiji vya Tutuo, Mlogolo, Mkolye, Tumbili na
Sikonge mjini na mifugo kukosa maji, hali ambayo itafanya mifugo mingi kufa.
Kutokana na hali ilivyo Bw. Jafari aliwasihi
wananchi kujiepusha na uharibifu wa mazingira kwa kukata miti ovyo ili kulinda vyanzo vya maji katika maeneo
yaliyo mengi na akawashauri wananchi hao wageukie kilimo cha mazao ya msimu
kama vile mhogo, viazi vitamu, alizeti na wale walioacha kulima tumbaku waanze
sasa kulima pindi mvua zitakapoanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Bw. Paul
Nkulila, akizungumzia hali hiyo, alikiri kuwa hali si shwari katika maeneo mengi kwani mvua
imekuwa kidogo sana, na kubainisha kuwa katika
bwawa la Ulyanyama maji yamekaribia kukauka kabisa na yaliyobaki ni machafu
sana hayafai kwa shughuli yoyote ya kilimo.
Bw. Nkulila
aliongeza kuwa baada ya kuona hali ya mvua siyo nzuri, na kugundua upungufu uliopo
wa tani 2700 za chakula, waliwatahadharisha
wananchi kutouza chakula chote, sambamba
na kuwashuri kuchukua hatua hasa kwa kugeukia kilimo cha mazao mbadala
yanayostahimili ukame, na akabainisha kuwa jitihada zinaendelea za kuwatafutia
mbegu za mazao kama vile mtama na mhogo.
…. ‘‘Tunataka kuchukua mbegu za mhogo toka kituo cha
utafiti cha Malugu kilichoko mkoani Kagera kwani hili ni zao mbadala linaloweza
kustahimili ukame na kuwa msaada mkubwa
katika wilaya yetu’’, alibainisha Bw. Nkulila
Bw. Nkulila aliongeza kuwa tayari halmashauri
imeshaomba chakula cha msaada toka serikalini, na akabainisha kuwa mda si mrefu
watapata tani 113 za mahindi ya ruzuku na tani 13.5 za mahindi ya bure, na yote
yatatolewa kwa familia zilizothibitishwa kuwa na upungufu katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment