Pages

KAPIPI TV

Tuesday, December 4, 2012

AJALI MBAYA IRINGA LEO,WANNE WAPOTEZA MAISHA

    Mkuu  wa nchini (IGP) Said Mwema
Ajali  mbaya  imetokea  mkoani Iringa mchana  wa  leo na kusababisha  vifo  vya  watu  wanne  wa familia  moja .
 

Ajali  hiyo  imetokea katika  eneo la geti la mafundi wa kutengeneza barabara  kuu ya Iringa -Mafinga  mkoani Iringa.

Kwa mujibu  wa mashuda  wa  tukio   hilo  wameeleza  kuwa  chanzo  cha ajali  hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 kuendesha  kwa mwendo kasi na kushindwa  kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.
 

Aidha katika ajali  hiyo  abiria  wote  wanne akiwemo baba,mama  na  watoto  wawili  waliokuwemo katika gari  hiyo ndogo wamekufa papo hapo ambapo maiti  zote tayari zimekwisha pelekwa  Hospitali ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya kuhifadhiwa.
 

No comments: