Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe ya mjini
Zanzibar, leo imetoa fursa ya dhamana kwa Viongozi wa makundi mawili ya
kidini Zanzibar wanaotuhumiwa kwa makosa ya kufanya fujo na kupelekea
ghasia na vitendo vya uvunjifu wa amani na uharibifu wa miundombinu ya
barabara.
Watuhumiwa
hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikhe, Faridi Hadi
Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe, Mselem Ali Mselem,
Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali
Suleiman na Hassan Bakar Suleiman.
Akisoma
uwamuzi huo huku kukiwa na ulinzi mkali eneo lote la Mahakama, Hakimu
wa Makahama hiyo Mh. Msaraka Pinja, amesema kuwa ingawa upande wa
Mashtaka ulikuwa haukutoa pingamizi ya dhamana kwa watuhumiwa, lakini
Mahakama ililazimika kusitisha utoaji dhamana baada ya kupitia mambo
kadhaa ya msingi.
Amesema
kuwa pamoja na uzito wa tuhuma zinazowakabili watuhumiwa, Mahakama
ililazimika kusita kutoa dhamana kwanza kwa usalama wa watuhumiwa
wenyewe na kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo wakati huo na uwezekano
wa kuingilia upelelezi wa kesi inayowakabili.
Hakimu
huyo alisema wasiwasi wa Mahakama ilikuwa kwamba watuhumiwa hao wakiwa
nje ya dhamana kuna uwezekano wa kutenda kosa lingine, Kutohudhuria
Mahakamani kwa wakati wanapotakiwa na kuangalia kwa mapata uzito wa kosa
wanaloshitakiwa nalo.
Baada
ya kuridhika na Mahakama hiyo ilitoa dhamana kwa watuhumiwa wote saba
kwa mashariti ya kuwasilisha mahakamani fedha taslimu kiasi cha shilingi
milioni tatu kwa kila mmoja pamoja na kuwa wadhamini watatu ambao ni
watumishi wa Serikali kwa kila mmoja akitoa kiasi kama hicho cha fedha
mahakamani.
Watuhumiwa
hao pamoja na Wadhamini wao, kwa pamoja wametakiwa kuwasilisha barua
kutoka kwa Sheha wa Shehiya anayoishi pamoja na kivuli cha vitambulisho
vya Zanzibar Mkazi na kwa wale wenye Hati za Kusafiria pia wawasilishe
vivuli vya hati hizo Mahakamani.
Pamoja
na masharti hayo ya jumla, lakini pia wadhamini wometakiwa wawe
watumishi wa serikali na wawakilishe barua kutoka katika ofisi
wanazozifanyia kazi na vivuli vya vitambulisho vyao vya kazi ili view
kama kumbukumbu mahakamani.
Hata
hivyo watuhumiwa wote wamerejeshwa rumande baada ya kushindwa
kutekeleza masharti ya dhamana pamoja na kukabiliwa na kesi nyingine
Mahakama Kuu ya Vuga, kesi ambayo dhamana yake imewekewa pingamizi kwa
hati maalum ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar kwa sababu za kiusalama.
Kesi hiyo imeahirishwa tena hadi Novemba 21, mwaka huu itakapotajwa tena.
Akizungumza
mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo mmoja ya Mawakili wa
Watuhumiwa hao Bw. Abdallah Juma, amesema yeye pamoja na wakili mwenzake
Bw. Salum Toufik, wataendelea kuwatetea watuhumiwa hao hata baada ya
kutishia kujitoa katika kesi hiyo mwezi uliopita.
0784 886488, 0715 886488, 0767 886488 Insp. Mhina
No comments:
Post a Comment