Na Hastin Liumba, TABORA
CHAMA cha wanawake wataalamu wa kilimo na mazingira, (TAWLAE), kimefanikiwa katika majukumu yao ambapo sasa kimefikia hatua ya kuwa na wanachama zaidi ya 600 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
Akitoa
taarifa yake kwenye mkutano wa chama hicho wa kumi na sita mkoani
Tabora, Sophia Mlote, alisema kilisajiliwa rasmi mwaka 1995 kikiwa na
wanachama 50 wenye fani mbalimbali zikiwemo Kilimo, Mifugo, Mazingira na
Maliasili.
Alisema
chama hiki kimekuwa na shughuli nyingi za kimaendeleo ikiwemo
kumwendeleza mwanamke mtaalam katika sekta ya kilimo, mifugo, maliasili
na mazingira.
Mlote
alisema kuwa chama hicho pia kimeazimia kukomesha tabia ya jamii kadhaa
kutumikisha watoto mashambani na badala yake waende shule wakasome
kwani elimu ni msingi wa maisha yao ya baadaye.
Aidha
Mlote aliongeza kuwa majukumu mengine ya chama ni kuhamasisha na
kuboresha kilimo cha mazao kama mihogo, viazi vitamu na mboga mboga
pamoja na usindikaji na uhifadhi wa mazao hayo.
“Hizi
sekta ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya mwanadamu na hasa akina mama
kwani huingiliana na mazingira haya kila aamkapo.....kipekee chama hiki
kinashughulika na kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti na kuhifadhi
mikoko katika ukanda wa pwani”. Alisema Mlote.
Akizungumzia
baadhi ya kazi za chama hicho alisema kazi nyingine ni kuboresha mifugo
wakiwemo kuku wa kienyeji ili kuongeza lishe na kipato katika ngazi ya
kaya,kutoa ushauri nasaha kwa wasichana kuhusu elimu ya uzazi na
maambukizi ya ukimwi na kusimamia haki na sera ya wazee.
Aliongeza
kazi nyingine ni kusimamia miradi mbalimbali ya kitaifa na kimataifa
katika kuwaendeleza watoto, kutokomeza ajira mbaya kwa watoto na kutoa
elimu mbadala,kutoa elimu ya ujasiliamali ili kuongeza maarifa katika
kujipatia kipato.
Mlote
alifafanua kuwa chama kiliona umuhimu mkubwa wa kusomesha mtoto wa kike
anayekabiliwa na mazingira magumu kimaisha ambapo jumla ya wasichana
2177, wamepata ufadhili katika ngazi ya elimu ya sekondari na 580
wamefadhiliwa na katika ngazi ya elimu ya msingi.
Aidha, chama hiki kimesomesha akina mama ..... katika ngazi ya uzamili na uzamivu,ambapo baadhi ya wasichana waliomaliza sekondari wamefanikiwa kuingia katika vyuo mbalimbali vikiwemo vyuo vikuu.
Mlote
anaongeza kuwa zaidi ya watoto 10,125 wameondolewa katika ajira mbaya
na kurudishwa shuleni na wengine kupewa elimu mbadala,na lengo letu ni
kuwa na mkakati madhubuti na wa makusudi kuongeza idadi ya wanawake
katika soko la ajira.
Alisema licha ya
juhudi zote hizo katika kumuendeleza mwanamke chama kinakabiliwa na
changamoto ambazo ni uwezo mdogo wa chama katika kuwafikia wahitaji na
wanachama na kwa kiasi kikubwa chama kinategemea wafadhili katika
kutekeleza majukumu yake mbalimbali.
Aidha nyingine ni ugumu wa masharti kutoka kwa wafadhili wanaotoa misaada na kutokua na ofisi za kudumu za chama katika ngazi za taifa, mikoa na wilaya ili majukumu ya chama hiki yaweze kutekelezwa kama yalivyopangwa.
Aidha
aliomba serikali kuwapatiwa ufadhili endelevu kwa kushirikishwa katika
mipango ya Serikali inayotakiwa kutekelezwa na sekta binafsi na
mashirika yasiyo ya kiserikali katika mpango wa PPP (Public-Private
pertnership).
No comments:
Post a Comment