Kampuni
ya Sauti za Busara Zanzibar imesema kuwa haitaachana na Mwimbaji
Mkongwe wa Muziki wa Taarabu hapa nchini Bi. Fatuma Bint Mbaraska
maarufu kama Bi Kidude hata baada ya kutangaza kutaka kuachana naye.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo
inayoendesha Tamasha la kila mwaka la Sauti za Busara visiwani Zanzibar
Bw. Yusuf Mahmoud, imesema kuwa kamwe kampuni hiyo haitamtupa Bi.
Kidude.
"Wakati tunajuta kwamba baadhi ya watu wanaamini vinginevyo, tunatarajia kutamka na kuthibitisha tena kwamba tunatafuta na kuwafanyia wasanii kutoka Afrika Mashariki, Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla, itaendelea kumsaidia Bi. Kidude maisha yake yote". Imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Hata
hivyo taarifa hiyo imeongeza kuwa Busara Promotion iko tayari
kuzikabidhi fedha za Bi Kidude kwake mwenyewe ama kwa mtu ambaye
atatajwa na Bi. Kidude ili mradi kuwa makabidhiano hayo yatafanyika
kisheria yakiwahusisha mashahidi tena wakiwemo mwanasheria, mwakilishi
kutoka Serekalini na mbele ya Waandishi wa Habari ili kuepuka utata.
Hivi
karibuni, Sauti za Busara iliitisha mkutano na waandishi wa habari
Zanzibar ili kuelezea juu ya suala la muimbaji huyo hodari wa nyimbo za
utamaduni Bi Kidude ambapo ilitolewa taarifa ya mapato na matumizi ya
fedha za mwimbaji huyo zilizokuwa zikihifadhiwa na Sauti za Buisara.
Mkutano
huo uliohudhuliwa na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari,
uliitishwa kufuatia taarifa za kudhulumiwa kwa fedha kwa Bi Kidude
malalamiko ambayo yalikosa kujulikana chanzo chake.
Hata
hivyo katika mkutano huo ilibainika kuwa kuna watu walionyuma ya pazia
yaani mgongoni mwa Bi Kidude ambao wanamhitaji kwa lengo ls kumtsgfunis
frdhs zake kwa kujifanya wasamalia wema.
Waandishi
waliitaka Sauti za Busara kuendelea kumlea Bi Kidude na kuachana na
maneno ya mitaani ambayo yakishikiwa bango hayatakuwa na tija kwa Bi.
Kidude ama wanaojifanya wasamalia wema.
0715 886488/ 0784 886488
No comments:
Post a Comment