Pages

KAPIPI TV

Monday, November 19, 2012

BOMBA LA MAJI MACHAFU YALIYOKUWA KERO KWENYE MAKAZI YA WATU LAZIBWA -MUGUMU

BOMBA LILILOKUWA LIKITIRIRISHA MAJI MACHAFU YALIYOCHANGANYIKA NA
KINYESI LAZIBWA.
Na Anthony Mayunga-Serengeti
Novemba 19,2012.

HATIMAYE mamlaka ya mji mdogo wa Mugumu wilayani Serengeti umeziba
bomba lililokuwa likitiririsha maji machafu yaliyochanganyika na
kinyesi kwenda kwenye makazi wa watu na sehemu za biashara mtaa wa
sedeko.

Uzibaji wa bomba hilo umekuja siku chache tu baada ya gazeti la
Mwananchi kuripoti tukio hilo ambalo limepigiwa kelele ikiwa ni pamoja
na kuwasilishwa katika vikao vya baraza la madiwani bila ufumbuzi.

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Sedeco waliliambia gazeti hili kuwa siku
moja baada ya taarifa kutolewa hukuikionyesha picha ya tatizo hatua
ilichukuliwa haraka .

“Tunawashukuru sana waandishi wa habari maana tumeumia sana kwa muda
mrefu,mbunge amekuja mara mbili kapuuzwa ,baraza la madiwani
lilidanganywa lakini mmekuja hapa na kuandika na hatua zikachukuliwa
huku wakilaumu kwa nini tunawaambia waandishi,watendaji hawa hawafai
mpaka wasukumwe”alisema mmoja akina mama ntilie eneo hilo jina
limehifadhiwa.

Hata hivyo wakazi wa mtaa huo na wafanyabiashara walimtupia lawama
afisa afya wa mamlaka hiyo kuwa utendaji kazi wake ni mbaya kwa kuwa
wanapompelekea malalamiko anawajibu vibaya.

“Hatujui nafasi hizi wanazipataje maana ofisa afya wa mamlaka hii
hafai bomba liko mita kumi toka ofisi yake ,tunamweleza anatujibu kuwa
,harufu hiyo inawapunguzia bajeti ya kula kwa kuwa matumbo yatashida
yamejaa,tutegemee nini kwa mtumishi kama huyo analipwa kwa kazi
gani”alihoji Phinias Edward mfanyabiashara wa chakula eneo hilo.

Hata hivyo alipotafutwa kwa njia ya simu afisa afya huyo Chironge
Hamisi kutaka kujua utekelezaji wa kazi hiyo na malalamiko ya wananchi
aling’aka.
“Wewe walikuletea malalamiko ili tutengeneze hilo bomba,kwanza wewe
unaniuliza hayo wewe ni mkuu wangu wa kazi,mbona unaniuliza uliza haya
mambo unataka nini,wewe nini bwana”alijibu kwa ukali na kukata simu.

Hata hivyo ofisa mtendaji wa mamlaka hiyo Gidioni Obel alidai kuwa
matatizo yote hayo yanashughulikiwa kwa awamu na kuwa suala la bomba
wamemaliza ,lakini ukarabati wa choo ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo
ya maji kwa kuwa ilijengwa vibaya inahitaji bajeti kubwa na wakipata
fedha wataitekeleza.

Malalamiko ya wananchi wakiwemo wafanyabiashara ndani ya soko yalikuwa
ni utiririshaji wa maji machafu yaliyochanganyika na kinyesi kwenye
maeneo yao,huku baadhi ya wafanyabiashara wakilalamikia harufu mbaya
inayotokana na choo  hicho kutokuwa na mfumo wa kutolea hewa na maji .

No comments: