Pages

KAPIPI TV

Saturday, November 3, 2012

DC KUMCHAYA AWAKOMALIA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA

Na Hastin Liumba,Tabora

MKUU wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya,amewataka watumishi wa
halmashauri ya manispaa Tabora, kuwajibika ipasavyo katika kazi, kwani
zama za kutishiana maisha zimepitwa na wakati na kwamba umri alionao
hana sababu za kumwogopa mtu.

Kauli hiyo aliitoa kwenye kikao cha baraza la madiwani la manispaa
hiyo wakati alipokuwa akitoa salamu za serikali.

Kumchaya alisema zama za kutishana sasa zimepitwa na wakati na yeye
atafanya kazi zake bila ya kuogopa mtu wala kumuonea yeyote.

Aidha mkuu huyo wa wilaya alipiga marufuku wananchi ambao wamekuwa
wakichimba mchanga kienyeji bila ya kufuata taratibu.

“Kama kuna mtumishi yoyote hapa ananufaika ama anahisa na uchimbaji
mchanga sasa basi mazingira yanahabiwa sana.” Aliongeza.

Alisema taratibu za uchimbaji hazifuatwi na alimuagiza mkurugenzi wa
halmashauri ya manispaa Tabora,Sipola Liana kutoa vibali vya uchimbaji
mchanga kwa kufuata taratibu.

Aidha Kumchaya alionya pia wakazi wa manispaa wanaofuga mifugo yao
kuachana na tabia ya mifugo yao kuzurura mitaani hovyo na atakayekaidi
atachukuliwa hatua kali kwa kutozwa faini.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya alisitisha mara moja zoezi
la upimaji ardhi kwani limekuwa likieta usmbufu kwa wananchi hadi
kufikia hatua za kuandaman hadi ofisini kwake.

“Nasitisha mara moja zoezi la upimaji ardhi hadi fedha iwepo na
nikisikia kuna mtumishi yoyote amekwenda pima ardhi kinyemela
atamfukuza kazi mara moja.” Alisistiza.

Alisema Tabora matatizo ya ardhi ni zaidi ya asilimia 90 hivyo ameona
ni vyema kusitisha upimaji hadi hapo fedha za upimaji itakapokuwepo.

No comments: