Pages

KAPIPI TV

Friday, October 5, 2012

ZOEZI LA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA ZANZIBAR KUANZA OKTOBA 15, MWAKA HUU

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi- Zanzibar
Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa Zanzibar Bw. Vuai Mussa Suleiman, ameelezea utaratibu na ratiba ya usajili na utambuzi wa watu watakaopatiwa vitambulisho vya Taifa kwa upande wa Zanzibar.
Bw. Vuai ambaye alikuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wakiwemo wa Mtandao wa kutoa elimu juu ya Vitambulisho hivyo, amesema kuwa kazi hiyo itafanywa kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa kila mwenye sifa ya kupatiwa kitambulisho cha taifa anasajiliwa.
Amesema kuwa usajili huo utaanza rasmi Oktoka 15, 2012 Visiwani humo na ameitaja wilaya itakayoanza kuwa ni wilaya ya Kusini Unguja kuanzia siku hiyo hadi tarehe 26,10,2012.
Amesema wilaya ya kati zoezi litafanyika kuanzia tarehe 29.10.2012 hadi tarehe 9.11.2012 ikifuatiwa na wilaya ya Magharibi kuanzia tarehe 12.11.2012 hadi tarehe 23.11.2012.
Amesema wilaya ya mjini kazi ya usajili itaanza tarehe 26.11.2012 hadi tarehe 7.12.2012. Wilaya ya Kaskazini B. kazi hiyo itaanza tarehe 10.12.2012 hadi tarehe 21.12.2012 na Wilaya ya Kaskazini A. itafanyika Tarehe 24.12.2012 hadi tarehe 4.1.2013.
Bw. Vuai amesema kwa upande wa Pemba zoezi hilo litaendelea kwa kuanzia wilaya ya Mkoani tarehe 7.1.2013 hadi 18.1.2013. Wilaya ya Micheweni litafanyika kuanzia tarehe 21.1.2013 hadi tarehe 1.2.2013.
Amesema kuwa wilaya ya Wete zoezi hilo litaanza tarehe 4.2.2013 hadi tarehe 15.2.2013 na wilaya ya mwisho kwa upande wa Pemba itakuwa ni wilaya ya Chakechake ambayo itaanza zoezi hilo tarehe 18.2.2013 hadi tarehe 1.3.2013.
Bw. Vuai amewataka wananchi kujitokeza kuhakikisha kuwa wanasajiliwa kwa manufaa yao na ya taifa kwa ujumla.
Amewakumbusha wananchi kuwa na vielelezo mbalimbali vikiwemo vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya elimu ya msingi na Sekondari, vitambulisho vya bima ya afya ama mfuko wowote wa hifadhi za jamii ama leseni ya udereva, hati ya kusafiria, cheti cha mlipakodi kutoka TRA, ZRB.
Bw. Vuai amesema kuwa zoezi hilo halifungamani na itikadi zozote za kivyama, kidini na kwamba maafisa wake watawasajili wale wote watakao kuwa na vielelezo vyote ama kimojawapo kati ya hivyo.
Hata hivyo amesema kuwa usemi wa kuwepo vielelezo hauna maana kuwa mtu atakayekosa kielelezo hataandikishwa bali ataweza kuthibitishwa na Masheha ama viongozi wengine wa serikali za mitaa ama serikali za Vijiji na Vitongoji.

No comments: