ZANZIBAR
JUMATATU OKTOBA 22, 2012. Watuhumiwa saba kutoka Makundi mawili ya
kidini hapa Zanzibar, leo wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya
mikutano na kupelekea ghasia zilizoleta uvunjifu wa amani na uhalibifu
wa miundombinu ya barabara.
Waliofikishwa
katika Mahakama ya wilaya ya Mwanakwelekwe ni pamoja na Mwenyekiti wa
Jumuia ya Maimamu Zanzibar Sheikhe Farid hadi Ahmed(41) na Mwenyekiti wa
Kundi la Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselem(52).
Watuhumiwa
hao pamoja na wenzao wengine watano, walisomewa mashtaka ya kufanya
mikutano iliyopelekea fujo na uvunjifu wa amani kulikokwenda sambamba na
uharibifu wa miundombinu ya barabara na uharibifu wa mazingira kama
vile kukata miti na kuziba barabara.
Watuhumiwa wengine waliofikishwa mahakamani hapo ni MUSSA JUMA ISSA, AZAN KHALID HAMDAN,
SULEIMAN JUMA SUIMANI, HASSAN BAKARI SULEIMAN na KHAMISI ALI SULEIMANI ambao wote walikana mashitaka yao.
Mbele
ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwereke Mh. Msaraka Ame Pinja,
ilidaiwa na na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Bw. Maulidi Ame Mohammed,
kuwa kuwa watuhumiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kufanya mkutano na
kusababisha ghasia na vurugu hapo Septemba 27, mwaka huu.
Hakimu
Msaraka amekataa kutoa dhamana kwa Watuhumiwa hao hadi Alhamisi Oktoba
25, mwaka huu atakapofikiria kuwapa ama kutowapa dhamana watuhumiwa hao
kutokana na unyeti wa kesi inayowakabili.
Mbali
ya watuhumiwa hao wenye wafuasi wengi, lakini kivutio kikubwa leo
ilikuwa ilikuwa ni askari wa kutuliza Ghasia kinachojihusisha na masuala
ya ulengaji wa shabaha na udunguaji ambacho ni maalumu kwa kupambana na
vitendo vya ugaidi na majanga yasiotabirika.
Askari
hao wakiongozwa na naibu Mkurugugenzi wa makosa ya Jinai hapa Zanzibar
na Maafisa wengine wa Jeshi la Polisi, walionekana wakiwa wamesheheni
vifaa maalum vya kujikinga na risasi za moto na milipuko huku wakiwa
wamevalia kofia ngumu na miwani nyeusi zenye viona mbali.
Wengi
wao wakiwa wameketi kwenye magari yao na wengine wakishika doria katika
maeneo mbalimbali nje ya mahakama, wamewafanya watu waliofika
mahakamani hapo kusikiliza kesi za ndugu zao kubaki nje sio kwa woga
lakini wakiwashuhudia askari hao hadi watuhumiwa walipotoka na kupelekwa
gerezani.
Baadhi
ya wananchi walionekana wakiwauliza watu wengine siku ya kutajwa kwa
kesi hiyo baada ya muda wao mwingi kuishia kuwatazama Polisi hao
waliokuwa na silaha mbilimbli kwa kila mmoja mbali ya kuwa na mabom ya
gesi ya kutoa machozi
Lakini
pia kutojitokeza kwa watu wengi mahakamani hapo kunatokana na onyo la
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa aliyewataka wazazi na
walezi kuwazuia watoto wao kujihusisha na makundi yanayopelekea vujo na
vurugu.
Kamishna
Mussa alisema Askari Polisi kwa kushirikiana na wenzao wa vikosi
vingine vya Ulinzi na Usalama hapa Zanzibar, watahakikisha kuwa
wanapambana na yeyote atakayejihusisha na fujo na kuharibu miundombinu
ya barabara na mazingira.
Mji wa Zanzibar hivi sasa ni shwari na tulivu kana kwamba hakujatokea jambo lolote siku kadhaa zilizopita.
0715886488, 0784886488, 0767 886488
No comments:
Post a Comment