MJUMBE wa halmashauri
kuu ya CCM taifa,(MNEC),John Mchele,amesema pamoja na kupata nafasi hiyo,bado
hana nia ya kuwania ubunge kama inavyotafsiriwa sasa kuwa anajipanga.
Kauli hiyo
aliitoa jana kwenye hafla fupi ya kuwashukuru wanaCCM,na wananchi baada ya
kumpa nafasi aligombea ya ujumbe wa NEC wilaya ya Tabora mjini.
Hafla hiyo
ilihudhuriwa na watu zaidi ya 600 ambao ni wanachama wa CCM,viongozi wa madhehebu
ya dini,viongozi wa taasisi za serikali na wafanyabiashara.
Mchele pamoja
na kuweka rekodi ya mjumbe wa NEC wa kwanza toka wilaya ya Tabora mjini,alisema
pamoja na kutoa shukrani hizo kwa wanaCCM,nafasi aliyonayo anataka kuwatumika
wanachama wa chama cha mapinduzi kamwe hana wazo la kuogombea ubunge.
“Nafasi
niliyopata ya ujumbe wa NEC inatosha sitaki kujaza vyeo vingi pekee yangu
nataka na wanachama wenzangu wapate nafasi ya kukitumikia chama na wananchi…..nafasi
hii inanitosha sana ndugu zangu.”alisema.
Alisema atawatumikia
watu wote bila ya kujali makundi,itikadi za vyama kwani anatoka katika nafasi
ya uenyekiti wa TCCIA nafasi ambayo ni sekta binafsi.
Mchele aliongeza
kuwa anaipongeza na kuishukuru, CCM mkoa wa Tabora na taifa, kwa kuweza
kurejesha jina lake na hatimaye kuwa mjumbe wa NEC,na kamwe hatowaangusha
wanachama wenzake.
Hata hivyo
aliwataka wanaCCM wenzake mkoani Tabora kuachana na makundi ambayo yamekuwa
yakikimega chama cha mapinduzi na zaidi tukifanya mema watanzania wanayotarajia
tunaweza kuongoza dola milele.
Alisema kazi
ambayo anaamini sasa ni kujenga CCM mpya na iliyobora ili chama chetu kiweze
kuongoza dola kila chaguzi zinapowadia.
Alisema nafasi
aliyopata ataitumika vyema kwa kutoa ushauri wenye busara na kamwe makundi
yasipewe nafasi ya kuweza kuwapa hoja wapinzani kushambulia.
No comments:
Post a Comment