Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Imeelezwa
kuwa TV zote zikiwemo zile zenye migongo, matumbo zote
zina uwezo sawa wa kupokea matangano ya digitali na Watanzania waepuke
uvumi wa watu wachache wanaodai kuwa TV za zamani hazitapokea zitafutwa
mara Tanzania itakapoingia kwenye mfumo wa Digitali.
Wito
huo umetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano hapa
nchini TCRA ambaye pia na Mratibu wa Ofisi za Kanda Bw. Victor Nkya,
wakati wa mkutano wa Wataalamu wa Mawasiliano ya Habari kwa njia ya
digitali kutoka nchi za SADC unaojadili umuhimu wa mfumo wa Digitali.
Bw.
Nkya amesema kuwa wananchi hawana haja ya kuwa na hofu juu ya TV
walizonazo zikiwemo zenye matumdo na migongo mikubwa kuwa hazitaweza
kupokea matangazo ya televishen katika mfumo mpya wa digitali.
Amesema
kutokana na watu wengi kutumia televishen za Analojia, ni lazima kila
mmoja wetu awe na kingamuzi na kazi ya Mamlaka ya mawasiliano ni
kuwajengea wananchi matumaini na kuepuka kudanganywa.
Kwa
siku za hivi karibuni baada ya Tanzania kuridhia mabadiliko ya mfumo wa
Digitali, wananchi wamekubwa na wasiwasi wakidhani kuwa huo ndio mwisho
wa tv za zamani.
Awali
akifungua Mkutano huo wa siku tatu hapa mjini Zanzibar, Waziri wa
Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mh. Rashid Suleiman, amewataka
wananchi kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa
mabadiliko ya kutoka katika mfumo wa analojia na kuingia katika
digitali.
Amesema
ni vema wananchi wakahama mapema kutoka katika mfumo huo wa zamani ili
kuepuka usumbufu wakati yatakapotokea mabadiliko hayo kwani hakutakuwa
na muda wa nyongeza kama Watanzania walivyozoea.
Na
kuna umuhimu wa wananchi pia kusikiliza maelekezo ya wataalamu badala
ya kusikiliza propaganda za watu wasio na ujuzi juu ya teknolojia hiyo.
"Watanzania
hawana haja ya kuogopa na badala yake wajiandae kujipatia vingamuzi na
kinyume cha hivyo watashindwa kupata matangazo ya televishen kama
wanavyotarajia." Alisema Waziri.
Amesema
kila mabadiliko yana hasara na faida zake, lakini kwa mabadiliko ya
kutoka katika mfumo wa analojia kwenda digitali, kuna faida kubwa na
moja ya faida hizo ni kuwawezesha watu wote kupokea matangaza sawa na
yenye ubora unaofanana na kwa wakati muafaka.
Mkutano
huo wa siku tatu unazishirikisha nchi zote za Jumuiya ya Maendeleo ya
Kusini mwa Afrika SADC ikiwemo Angola, Afrika ya Kusini, Malawi,
Namibia, Botswana, Swazlland, Lesotho, Msumbiji na wenyeji Tasnzania.
No comments:
Post a Comment