Pages

KAPIPI TV

Monday, October 22, 2012

MAJAMBAZI WALIVYOTUADHIBU

Nilipoimbishwa mtaji wa masikini bila kupenda!...
Nassor Wazambi
Nilipoimbishwa mtaji wa masikini bila kupenda!

Ijumaa tar.12/10/2012 nilikutana na tukio ambalo sikuwahi kukutana nalo zaidi ya kuhadithiwa. ilikuwa majira ya saa mbili na robo usiku nikitoka sikonge na rafiki yangu kuja tabora mjini tukiwa na pikipiki, tulipofika maeneo ya mtakuja ukipita kidogo mnara wa simu, tukakuta barabara imefungwa kwa kuwekewa mawe makubwa na magogo yaani hakuna hata pakupita baiskeli, hatukuwa najinsi tukasimama, rafiki yangu aliekuwa anaendesha baada yakuona hakuna mtu aliamua kugeuza pkpk turudi tulikotoka lilikuwa kosa kubwa! waliibuka watu kutoka kila upande nakuaanza kutushushia kipigo mwenzangu alipigwa pigomoja tu zito akapoteza fahamu! bahati mbaya sana kabla hajazimika alisema "boss wameniua!" hapo ndipo aliponiponza maana wazee wote sita walihamia kwangu ilikuwa kipondo mfululizo huku niki sachiwa kila sehemu inayoweza kukaa hela, mbali yakuchukua hela zote, cm, na camera nililazimishwa na kutaja namba ya siri ya Mpesa!


cha ajabu!

tuliwekwa chini ya ulinzi zaidi ya saa nzima, hakuna hata gari moja lililotokea wala mlinzi wa mnara mbapo ni jirani na tukio lilipotokea hakuhangaika japo kujulisha police.

shukrani!

nawashukuru wazee wale wa kazi (waliotuteka) maaana walitupa vitu vyetu muhimu wakati wanatuachia kama kadi za benki, leseni zote mbili, vitambulisho, pia wakatupa tsh. 15,000 tukaongeze mafuta maana yalimwagika mengi wakati pkpk imelala chini!
kwa sasa maumivu yameisha niko fiti kabisa

No comments: