Kumwami Mwongezya akiwa chini ya ulinzi wa Polisi |
Na Juma Kapipi-Tabora
Diwani
wa CCM kata ya Igigwa wilaya ya Sikonge Saada Said Sizya amejikuta
akimkwida mtu mmoja kwa kutapeli kiasi cha Shilingi mil.moja na laki
mbili akidai kutumwa na hakimu ili aweze kufuta kesi inayowakabili watu
26 waliokamatwa ndani ya hifadhi ya Nyahua iliyoko wilayani Sikonge.
Katika
tukio hilo lililokuwa kama mchezo wa sinema eneo la Mahakama ya hakimu
mkazi Tabora,diwani huyo Saada Sizya ambaye alifika kwa lengo la kutaka
kuwasaidia watuhumiwa hao 26 wanaoishi eneo la Mwamsonga lililopo kwenye
kata yake alipata habari kutoka kwa mmoja kati ya ndugu waliofika
mapema mahakamani kwa hatua zaidi za kushughulikia kesi hiyo kuwa tayari
kuna mtu wamekwisha mpatia kiasi cha shilingi mil.moja na laki mbili
alizodai ametumwa na hakimu anayeshughulikia kesi hiyo ili watuhumiwa
hao waweze kuachiwa huru.
Saada Said Sizya diwani kata ya Igigwa-Sikonge |
Hali
hiyo ilimtia mashaka diwani huyo na kutaka aoneshwe mtu huyo ambaye
alifahamika kwa jina la Kumwami
Mwongezya(60),ambapo sasa diwani Saada
alitupa mkoba wake pembeni na kumkwida huku akiomba msaada kwa askari
Polisi waliokuwapo mahakamani hapo.
Hata
hivyo mtu huyo Kumwami ambaye ni mkazi wa kata ya Ilolangulu alijaribu
kujitetea kwa diwani huyo huku akimvutia pembeni ya eneo la mahakama
alitoa kiasi cha shilingi elfu hamsini za noti ya elfu kumi kumi huku
akiomba wazungumze kimyakimya jambo ambalo lilidhihirisha kuwa mtu huyo
ni kweli amechukua kiasi hicho cha fedha.
Baada
ya askari Polisi kumkata na kumfunga pingu Kumwami alikiri kuchukua
kiasi cha shilingi mil.moja na laki moja taslimu na laki moja iliyobaki
aliipokea kupitia M-pesa kwa madai ya kusaidia kutoa hongo ili kufuta
kesi ya watuhumiwa hao 26 wanaokabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la
kuingia na kuweka makazi ndani ya hifadhi ya msitu wa Nyahua kinyume cha
sheria namba 14 ya mwaka 2002 kifungu 84(1)(a) na (5).
Licha
ya kukubali kutenda kosa hilo la utapeli Kumwami hadi anatolewa
mhakamani hapo kupelekwa kituo cha Polisi ili akafunguliwe jarada lakini
hakuwa tayari kumtaja hakimu aliyemtuma kufanya hivyo.
Aidha
kwa upande mwingine watuhumiwa hao wapatao 26 wakiwemo wanawake watano
na wanaume 21 walilirudishwa mahabusu baada ya kusomewa mashitaka matatu
na mwanasheria wa serikali Miraji Kajiru mbele ya hakimu mkazi Jocktani
Rushwela ambaye aliisogeza mbele kwa muda wa siku moja kesi hiyo kwa
madai ya kusubiri ushahidi upande wa mashtaka.
No comments:
Post a Comment