Pages

KAPIPI TV

Tuesday, October 2, 2012

CCM YAPATA JEMBE LA UHAKIKA TABORA... NI JOHN MCHELE MJUMBE WA NEC

 Mjumbe wa NEC Bw.John Mchele.

"Haikuwa rahisi kuamini kwamba hivi huyu John Mchele ndiye sasa ni mjumbe wa NEC ya CCM au ni utani"...Haya yalikuwa baadhi ya maneno ya wadau mbalimbali mjini Tabora kwa kuamini kuwa John Mchele ni mtu makini na ambaye akidhamilia kufanya jambo fulani na tena lililo na maslahi  kwa jamii huwa harudi nyuma hadi kupatikana kwa mafanikio au la sivyo jua litachomoza na kuzama hadi kieleweke.

Kwa wakati mwingine pia ilikuwa ni mshangao kwa baadhi yao ambao waliwahi kumshawishi hata kugombea Ubunge katika chaguzi zilizowahi kufanyika hasa wa mwaka 2000,2005 na 2010 lakini John Mchele hakuwa tayari kufanya hivyo na wala kuonesha dalili zozote za kujitosa katika kinyang'anyiro chochote ndani ya CCM kwa wakati huo.

Binafsi najaribu kujiuliza hivi John Mchele inawezekana kuwa kuna mtu alimshawishi kuingia kwenye ulingo wa siasa na kuacha Shughuli zake nyingine za kawaida?au amekwisha fikia uamuzi wa kuingia kwenye siasa kwa wakati huu ambao kumekuwa na mivutano ya mara kwa mara baada ya kuzuka kwa makundi ndani ya CCM?

Kwahili napingana nalo,kwakuwa John Mchele ninavyomfahamu si mtu wa makundi,si mtu wa kushawishiwa kuingia kwenye migogoro,na wala si mtu wa kulipizana kisasi na mtu aliyemkosea na kwa uthibitisho wa hili ni pale John Mchele alipowahi kushika nyadhifa mbalimbali za ngazi za mkoa hasa kwenye vitengo vya Taasisi za wafanyabiashara na wasafirishaji,jambo ambalo ilidhihirika kuwaunganisha wanachama katika Taasisi hizo na Serikali hatua ambayo iliondoa migongano iliyokuwa imedumu kwa muda mrefu pasipo ufumbuzi.

Na hata nilipojaribu kungia mitaani ili nipate sifa mbaya ya John Mchele, napo niligonga mwamba baada ya kila mmoja niliyebahatika kuzungumza naye alinihakikishia kuwa John Mchele ni Mjamaa wa Kweli kwa shida na raha,...."Anashiriki kwa hali na mali shughuli za kijamii mitaani,Ukiwa na shida binafsi hata kama hana uwezo wa kukusaidia ujue atakupa hata ushauri ambao utakusaidia kuondokana na dhahama iliyokukumba"ni maneno ya mmoja kati ya watu wa mjini Tabora.

HIVI KWANINI JOHN MCHELE KACHAGULIWA KUWA MJUMBE WA NEC YA CCM
Hapa sioni sababu ya kufikiria sana kwani kwa haya yote niliyokumbana nayo huko mtaani,maofisini na hata kwa wafanyabishara Sokoni, naamini CCM kwa umakini wake huko Dodoma iliamuliwa kati ya majina matano yaliyorudi ni pamoja na la John Mchele baada ya kupimwa na kikao kizito ambako vigogo ngazi ya juu wa CCM Taifa walifanya maamuzi hayo.

Sitaki kuzungumzia uchaguzi uliomuweka katika nafasi hiyo ya ujumbe wa NEC ambao ulifanyika katika ukumbi wa Chuo cha utumishi wa Umma au Uhazili ambako kulikuwa na patashika ingawa nguo hazikuchanika John Mchele akaibuka mshindi hata sasa kwa hatua hiyo anaanza kutambulika kuwa ni kiongozi halali ngazi ya juu ya CCM ingawa wapo watu hawakupenda litokee hilo.

Jitihada zake katika kuonesha ni jinsi gani naye anaweza kuwaongoza  wana CCM wenzake na hasa mchango wake makini unahitajika sana wakati huu wa mfumo wa vyama vingi kwakuwa ili CCM iweze kushinda inahitaji ipate watu wabunifu,Waaminifu na Waungwana kama John Mchele na hasa inapofikia wakati wa Uchaguzi mkuu nchini.

Lakini pia nikirudi nyuma nazidi kuufikiria uvumi ambao umezagaa mkoa mzima wa Tabora,Eti wanaCCM wenyewe wanasema muda umefika wa kuwapa Uongozi watu ambao wanaishi yaani WANALALA NA KUAMKA WAKIWA TABORA na si wale WANAOISHI DAR-ES-SALAAM WANAKUWA WAKARIMU SANA WAKATI WANAPOKUJA TABORA KUTAFUTA UONGOZI na baada ya hapo maisha yao ni Dar-es-Salaam.

"Kwakweli tunazidi kudharaulika sana utadhani hapa hakuna watu kabisa wanaoweza kuongoza!,sasa tumechoka,tunawaambia walioko nje ya Tabora....HAPA SIO SHAMBA LA BIBI"....Haya sio maneno yangu ni wadau wa Tabora hao wameamua kufunguka.

Maamuzi ya John Mchele kuamua kujitosa katika kinyang'anyiro hicho ulipokelewa kwa Shangwe na wanaCCM waliowengi na kuweza kumuhakikishia John aone kuwa kumbe hata mtu asiyefahamika na wengi na tena ambaye hajawahi kugombea nafasi yoyote katika Chama anaweza kuwa kiongozi na akafanya vitu zaidi ya yule ambaye ana jina kubwa na fedha kibao.

"NAWAPONGEZA  WOTE WALIONICHAGUA NA WASIO NICHAGUA KWANI WAMETUMIA DEMOKRASIA YA KWELI"...Hayo ni maneno ya John Mchele huku akisisitiza kuwa na umoja miongoni mwa wanaCCM wote. 
     


          

No comments: