Zitto alisema
hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya
kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la
Mwanga, mjini Kigoma.
Zaidi ya watu
200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali
mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto
anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.
“Nimefanya kazi
kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni
mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza
kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi.
“Kama Mungu
ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya
inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha
Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya
kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.
“Nataka kuleta
changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za
msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu.
“Iwapo chama
kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani
urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni
vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.”
Atangaza kugombea urais
Atangaza kugombea urais
Katika hatua
nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
“Kwanza nataka
niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi
hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea.
Hata hivyo Zitto
alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo
kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo
wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na
ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika
katiba mpya.”
“Nchi za
Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo
katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,”
alisema Zitto
Katika kukazia
hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976
uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001,
Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia
56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46.
Katika hatua
nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila
akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa.
“Ndugu zangu
naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama
cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya
kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.
“CCM imewahi
kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha
Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto.
Alisema ili
kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010,
Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura
nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia
nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.
No comments:
Post a Comment