![]() |
| Wanafunzi Singida |
Na.Nathaniel Limu-Singida.
Mtihani
wa kumaliza elimu ya msingi unaohusisha wanafunzi 27,749 wa darasa la
saba mkoani Singida umeanza kwa amani na utulivu licha ya kujitokeza
kwa kasoro ndogondogo.
Miongoni
mwa kasoro hizo ni pamoja na utoro, baadhi ya wanafunzi kutojua
kusoma na kuandika na walimu na wasimamizi kulalamikia mfumo wa maswali
ya kuchagua na kuweka vivuli.
Katika
shule ya msingi Mtisi iliyopo umbali wa zaidi ya kilomita 24 kusini
magharibi mwa mji wa Singida, wasimamizi wa mtihani huo wamesema kati
ya 34 watahiniwa nane (8) hawakufanya mtihani kutokana na utoro na
wengine sita wameshindwa kusoma wala kuandika.
Hata
hivyo afisa elimu mkoa wa Singida Yusuf Kipengele, amesema mbali ya
kasoro hizo hakuna dosari nyingine kubwa iliyojitokeza na kuathiri
ufanyaji huo wa mtihani ulioanza leo.
Kipengele
ametoa wito kwa wasimamizi wa mtihani huo kuwa waadilifu na
kutojihusisha na udanganyifu vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria
pindi watakapobainika.



No comments:
Post a Comment