Pages

KAPIPI TV

Tuesday, July 24, 2012

NYUMBA SABA ZACHOMWA MOTO SIKONGE KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MTOTO WA MIAKA MINNE"Aliuawa na baadaye kubanikwa akiwa amekatwa mikono na miguu"

Mkuu wa wilaya ya Sikonge Hanifa Selungu
 
Na Lucas Raphael,Sikonge

Nyumba zachomwa moto

NYUMBA saba za familia nne katika Kijiji na Kata ya Usunga wilayani Sikonge zimechomwa moto kutokana na kutuhumiwa mauaji ya mtoto Fanuel Enock(4) aliyepotea tarehe 9 na kupatika Jumanne mwezi huu akiwa hana mkono na mguu huku mwili wake ukiwa umekaushwa.

Diwani wa Kata ya Usunga.Mariam Ukongom,amesema wananchi walitangaziwa kupotea kwa mtoto huyo na mwili wake ulipopatikana walichukua sheria mikononi kwa kuzichoma nyumba za familia hizo moto wakizituhumu kushiriki kumuua mtoto huyo kwa imani ya kupata utajiri.

Alisema kwamba kitendo cha wananchi hao kujichukulia sheria mikononi kinafanya jamii kwenda mabli sana kwani kitendo hicho ni cha kinyama sana kwa kukatiliwa watu wengine makazi yao kisa ni imani za kishirikina.

Ameutaka uongozi wa wilaya ya sikonge kuwachukulia hatua kali wale wote walioshiriki kufanya vitendo hivyo vya ukatilia uliofanyika kwa wananichi wasiokuwa na hatia.

Mkuu wa wilaya ya sikonge, Hanifa Selungu,amewataka wananchi wilayani Sikonge kuachana na imani za kishirikina zilizojengeka miongoni mwao na kama kuna tuhuma za mauaji vyombo vya Dola viachwe vifanye kazi yake.

Alisema kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu wote waliofanya vitendo hivyo vya kinyama na kufikishwa kwanye vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zaidi.

Mkuu huyo wa wilaya ya sikonge alisisitiza kwamba hataki kusikia katika wilaya hiyo wananchi wanajichukulia sheria mikononi bali watoe taarifa ili hatuan ziweze kuchukuliwa dhidi wa watu wanatuhumiwa .

No comments: