Na Salma Said,
Waziri
wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad
amejiuzulu wadhifa wake leo jioni imeelezwa. Kwa mujibu wa taarifa ya
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid
Yahya Mzee ilisema tayari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud
kujiuzulu.
“Tarehe 20
Julai,2012 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mheshimiwa Hamad Masoud
Hamad alimuandikia barua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohammed Shein ya kumuomba ajiuzulu kufuatia ajali
ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit iliyotokea Julai 18,2012” Ilisema
taarifa ya Dk. Mzee.
Kufuatia
kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais Dk Shein amemteua Mwakilishi wa Jimbo
la Ziwani(CUF) Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na
Mawasiliano.
“Kufuatia
kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano,Rais
amemteua Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na
Mawasiliano” Taarifa ya Ikulu ilisema.
Uteuzi wa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano umeanza Julai 23 mwaka huu.
Wakati huo
huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali
Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya
Mv. Skagit.
Mwenyekiti wa
Tume hiyo ni Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wajumbe ni Meja Jenerali S.S.
Omar, COMDR. Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein
Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq, Kaptein Hatibu Katandula, Bi.
Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu
wa Tume.
No comments:
Post a Comment