.
Na Berensi Alikadi-Bunda.
WILAYA ya Bunda mkoani imekamilisha
zoezi la usaili wa makarani wa sensa watakaohusika katika kazi ya
kuhesabu watu katika wilaya hiyo Agost 26 mwaka huu.
Mwenyekiti wa kamati ya sensa ya wilaya hiyo Joshua Mirumbe amesema jana
kuwa zoezi hilo limeenda vizuri katika vijiji vyote vya tarafa nne za
wilaya
hiyo ambazo ni Nansimo,Kenkyombyo,Chamliho na Serengeti.
Joshua ambaye pia ni mkuu wa wilaya
hiyo amesema kuwa kilichobaki
sasa ni kuyachambua majina hayo na kuona wale waliokidhi vigezo ambao
alisema
kuwa ndio watakaochukuliwa kwa ajili ya
kufanya kazi ya sensa na wala si vinginevyo.
‘’Pamoja na kufanya usaili huo
kilichobaki sasa ni kuchanbua
majina ya wale waliokidhi vigezo tu ndio watakaochukuliwa maana hili
zoezi ni
la kitaifa hatuwezi kuchukuwa kila mtu hata wale wasiokuwa na sifa maana
likiharibika ni aibu kwa wilaya yetu.’’alisema Mirumbe.
Alifafanua kuwa baada ya kamati ya
wilaya kupitia majina
hayo na kuchagua yanayofaa yatapelekwa katika vijiji husika kwa ili
waliochaguliwa waweze kujiandaa kwa ajili ya semina ambayo alisema
itaanza muda
si mrefu. Katika tarafa zote nne za wilaya hiyo.
Aidha mwenyekiti huyo alirudia wito
wake wa kuwataka
viongozi wa dini. Vyama ,mashirika yasiyokuwa ya kiserikali,maafisa
tarafa
watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha wanahamasisha wananchi ili
waweze
kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo
.
Alitoa
onyo kwa mtu yeyote au kikundi cha watu ama dhehebu
la dini litakalogomesha zoezi hilo
litachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja
na kufikishwa mahakamani kwani atakuwa amevunja sheria ya takwimu sura
ya 351.
Alisema kuwa kwa zoezi hili serikali
haitamuonea aibu mtu
yeyote atakayeonekana anania ya kukwamisha zoezi hilo
hivyo ni vema wale wenye mawazo hayo wakaacha mapema kwani serikali
imejiandaa
kukabiliana na wote wenye nia ovu kuhusu zoezi hilo .
No comments:
Post a Comment