Afisa Mtendaji mkuu wa benki ya CBA, Bw Yohane Kaduma akimkabithi mfano
wa hundi yenye thamani ya Tsh Millioni 5 kwa makamu wa pili wa Raisi wa
Zanzibar Balozi Seif Idd, Afisa Mtendaji Mkuu wa CBA Bw Kaduma amesema
benki yake iko tayari kuikopesha serikali ili iweze kununua meli mpya
ili kuhakikisha inaboresha huduma za usafiri majini.Nae balozi Seif Idd
ameshukuru msaada huo kutoka CBA na ametoa wito kwa wadau mbalimbali na
serikali kuitembelea benki hiyo ili kuona ni jinsi gani taifa linaweza
kufaidika hasa kwenye kuisaidi serikali kuboresha usafiri majini
Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Wakati
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa kwenye mchakato wa kutafuta
fedha za kununua meli mpya, Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), imesema
iko tayari kuikopesha SMZ fedha za kununulia Meli hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Yohane Kaduma, amesema benki yake iko
tayari kuipitia SMZ mkopo wa kununulia Meli hiyo endapo watakubaliana na
kushirikishwa kwenye mchakato huo.
Bw.
Kaduma alikuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zannzibar mara
baada ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni 5, kwa Makamu wa pili wa
Rais wa Zanzibat Balozi Seif Ali Iddi ili kusaiidia ghala za matibabu
kwa majeruhi na ubani kwa wafiwa wa ajali ya Meli ya Skagit.
Bw.
Kaduma amesema kuwa endapo Benk yake itaombwa kutoa mkopo huo inaweza
kufanya hivyo ili mradi tu kukaa meza moja na Serikali na kukubaliana
aina ya mkopo pamoja na mambo mengine.
Awali
akipokea msaada huo, Makam wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, amesema
kuwa pamoja na kusimamishwa kwa baadhi ya meli za watu binafsi kuchukua
abiria, SMZ pia imeagiza meli zake kufanyiwa uchunguzi kama zinafaa
kuchukua abiria.
Balozi
Seif amesema kuwa ameziagiza Mamlaka ya usafiri majini Zanzibar na
Sumatra, kuzifanyia uchunguzi meli hizo za SMZ ikiwemo MV Maendeleo
ambayo imerejea siku za karibuni ikitokea Mombasa nchini Kenya ambako
ilikuwa katika matengenezo makubwa.
Amesema
Serikali haiwezi kukaa kimya huku ikiona kuwa wananchi wake wanapatwa
na majanga ya mara kwa mara kutokana na kusafiri kwa meli zisizo na
uhakika.
Katika
hatua nyingine idadi ya maiti za MV Skagit, imeongezaka hadi kufikia 128
baada ya maiti nyinine mbili kupatikana leo karibu na Kisiwa cha Chumbe
nje kidogo ya mji wa Zanzibar na nyingine sita zikipatikana mkoani
Tanga.
Tofauti
na taarifa za awali kuwa maiti tano zilipatikana Bagamoyo mkoani Pwani,
ifahamike kuwa maiti hizo zilipatikana katika fukwe za bahari wilayani
Pangani na nyingine mjini Tanga.
Kwa
mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani Tanga ACP Costantine
Masawe, maiti nne ikiwemo ya mwanamke mmoja zilipatikana huko Pangani na
nyingine mbili ikiwemo ya mwanamke mmoja zikapatikana kwenye fukwe za
bahari mjini Tanga.
Kamanda
Masawe amesema kuwa maiti zote zilichukuliwa vipimo kwa ajili ya
uchunguzi wa Vinasaba (DNA) pamoja na kupigwa picha kabla ya kuzikwa.
Hata
hivyo Kamanda huyo wa Polisi amesema kuwa maiti moja kati ya hizo,
ilitambuliwa kuwa ni ya Mohammed Saidi Salum mkazi wa Ziwani Chakechake
mkoa wa Kusini Pemba ambaye alitambuliwa baada ya simu aliyopatikana
nayo kufanyiwa uchunguzi.
Hadi
sasa maiti ambazo hazijapatikana ni 16 kutokana na kupatikana kwa watu
146 wakiwa hai ikilinganishwa na idadi ya watu 290 waliokuwemo ndani ya
meli hiyo ya Skagit siku ya tukio.
No comments:
Post a Comment