Pages

KAPIPI TV

Friday, July 6, 2012

AFISA MIFUGO MANISPAA YA TABORA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI USIKU"Ni moja kati ya mauaji ya mara kwa mara yanayofanyika mkoani Tabora"

 Mwili wa aliyekuwa Afisa Mifugo Manispaa ya Tabora Marehemu Severine Patrick Tesha,ambaye ameuawa  na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi eneo la Kanyenye nje ya nyumba ya kulala wa wageni inayofahamika kwa jina la Anna Lodge.

Mavazi  marehemu Tesha ambayo yametapakaa damu kutokana na mauaji hayo.

Na Mwandishi wetu Tabora.

Afisa mifugo wa halmashauri ya manispaa ya Tabora ameua kwa kupigwa risasi na watu ambao hawajafahamika wakati alipokuwa akirudi nyumbani kwake eneo la kata ya Kanyenye,barabara ya Kitunda majira ya saa saba usiku akitokea  matembezini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Anthony Rutha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuweka wazi kuwa marehemu Tesha majira hayo ya saa saba usiku alifika nyumbani kwake na kubisha hodi ili afunguliwe na mkewe.

Kamanda Rutha amesema wakati Tesha akifunguliwa mlango na mkewe alianza kupiga mayowe ya kuomba msaada kufuatia watu wawili waliokuwapo nje ya eneo la nyumbani kwake walipokuwa wakionesha dalili za kumdhuru hivyo Tesha akalazimika kukimbia ndipo watu hao walianza kumfyatulia risasi iliyompata kiunoni na hatimaye kufariki jirani na Anna Lodge alipokimbilia kutaka msaada zaidi.  

Pamoja na Kamanda Rutha kuomba msaada kwa raia wema kutoa taarifa za kuwafichua watu waliohusika na tukio hilo la kinyama alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa silaha iliyotumika ilikuwa aina ya Gobore linalotumia risasi za Shortgun ambapo eneo la tukio maganda matatu ya risasi yalipatikana huku akibainisha kuwa ni risasi moja tu ndio iliyompata Tesha na hata kusababisha umauti wake.

Hata hivyo Kamanda Rutha amesema hakuna mtu anayeshikiliwa hadi sasa kuhusiana na tukio hilo na huku upande wa ndugu wa marehemu Tesha ukieleza kuwa mwili wa marehemu unasafirishwa kwenda Moshi kwa ajili ya mazishi.  

No comments: