Na:Robert Kakwesi,Urambo
Wanakijiji wafunga ofisi ya kijiji
WANANCHI wa Kijiji cha kangeme,kata ya Zugimlole,wilayani
Urambo wameifunga ofisi ya kijiji wakishinikiza kusomewa Taarifa ya Mapato na
matumizi.
Wakizungumzia hatua hiyo wananchi hao walieleza umauzi wao
unatokana na uongozi wa kijiji hicho kutowsomea taarifa ya mapato na matumizi
kwa muda wa mwaka na mmoja na nusu.
Walisisitiza wataendelea kushikilia msimamo wao kwa vile
uongozi wa kijiji umekuwa ukiwapiga chenga wanapowasilisha ombi la kusomewa
taarifa ya mapato na matumizi.
Diwani wa kata ya zugimlole.Mh Moshi Kitoboli,alieleza
uamuzi huo wa wananchi unatokana na kutokuwa na imani na mwenyekiti wa Kijiji
hicho akisema haujasoma taarifa ya mato na matumizi kwa zaidi ya mwaka mmoja
sasa.
Alieleza uamuzi huo huenda unatokana na kamati ya maendeleo
ya kata kupanga ratiba na kuwajulisha wananchi kwa kufuata kalenda ya
halmashauri ambapo mkutano wa kusomewa taarifa ya mapato na matumizi ulikuwa
ufanyike tarehe 20 mwezi uliopita.
Ili kuweka mambo sawa,Diwani Kitoboli,alisema amemuagiza
Mtendaji wa Kata,George maganga,kufuatilia suala hilo na tayari yupo kijijini
hapo kupata ufumbuzi wa suala hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Urambo.Bi Anna Magowa,alieleza wiki kadhaa
zilizopita kuhimiza viongozi wa vijiji wilayani Urambo kusoma taarifa za mapato
na matumizi kwa kufuata kalenda za vikao.
Alisisitiza hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa wote
watakaokiuka agizo hilo jambo ambalo pia lilikubaliwa na baraza la madiwani
lilioafiki kuchukuliwa kwa hatua kwa watakaoshindwa kusoma taarifa za mapato na
matumizi.


No comments:
Post a Comment